Michu najua hujambo.
Hebu jamani nisaidieni katika ujenzi huu wa hii barabara ya mwendokasi.
Hapa ni makutano  ya barabara ya Morogoro Road na barabara ya mtaa wa Lumumba mbele ya Jengo lililochoka la Umoja wa Vijana ambapo ujenzi huu wa hii barabara unaendelea na nadhani uko katika hatua za mwisho.
Sasa tulivyozoea toka zamani mambo yalikuwa rahisi tu aidha ukitokea mjini au ukitokea magomeni au ukitokea Lumumba, mapito yalikuwa rahisi sana. Sasa kwa taswira hizi nilizochukua hapo leo, hivi inakuwaje katika mchangayiko huu.
Ndio kusema kwamba itakuwa msongamano hivi hivi unapofika junction hiyo au kuna maelekezo kutoka mamlaka zinazohusika? 

Mdau
Man U.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 16, 2013

    My God, how do you pass through there? Bongo must have excellent drivers if not there must be an accident every minute. I just can't believe people do actually manage to pass through.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 16, 2013

    Jamani mnamuuliza michuzi wakati yeye siyo mkandarasi wa hiyo barabara.Nendeni mkawaulize Strabag.Na pi huu siyo muda wa kuuliza hivyo kwani hao wanaojenga wanajua watafanya nn sehemu ambazo zina makutano kama hapo.Watz mna haraka kama nn.Tulieni barabara ikikamilika kama kuna mapungufu ndiyo mtayasema na siyo sasa wakati haijakamilika na kukabidhiwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...