Kampuni ya Tanzania Mwandi ikishirikiana na Majimaji FC, imeandaa mkutano wa wadau wote wa soka mkoani Ruvuma chini ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh. Said Mwambungu, mkutano utakaofanyika katika ukumbi wa Centenary tarehe 10. 08. 2013, kuanzia saa 2 asubuhi.

Lengo kubwa la mkutano ni kurejesha makali ya 1985, 1986 na 1998 kwa klabu ya soka ya Majimaji kwa kuiunda upya kiuchumi chini ya mfumo wa Kampuni, kuijengea uwezo wa kimkakati na kiuendeshaji ili iweze kushiriki kwa mafanikio Ligi Daraja la Kwanza na hatimaye kurejea Ligi Kuu msimu ujao.

Itakumbukwa kuwa Majimaji FC ni klabu ambayo imezalisha magwiji wengi wa soka Tanzania kama Abdala Kibadeni 'Mputa', Madaraka Suleimani 'Mzee wa Kiminyio', Peter Tino, Steven Mapunda 'Garincha', Hamis Gaga, Idd Pazi, Omary Hussein 'Machinga' na Mdachi Kombo na ni klabu ambayo ilikuwa na ushindani mkubwa kwa Simba na Yanga.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya Habari na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Mwandi, Bwana Teonas Aswile amewaalika wafadhili na wadau wote wenye mapenzi mema na Majimaji FC kujitokeza na kushiriki katika zoezi la mjadala wa muundo mpya wa Majimaji na hata kununua hisa kwani sasa Majimaji Kampuni haitakuwa na longolongo zozote.

“Binafsi nawahimiza wafadhili wa soka kwamba hii ni fursa adimu nyingine ya kuwekeza fedha zao mahali salama. Majimaji itakuwa ikiendeshwa kikampuni na miradi mbalimbali itaanzishwa na klabu ikiwemo upande wa ukandarasi na kuuza wachezaji nje ya nchi. Kwahiyo atakayenunua hisa atafaidika mara mbili.” alisema Teonas Aswile.

Akizungumzia wachokoza mada wakuu wa Majimaji Revival Conference, Aswile amesema kuwa Wakala wa Kimataifa wa FIFA na Mwanasheria Maarufu nchini, Dkt Damas Ndumbaro pamoja na Bwana Silas Mwakibinga, mhasibu na mdau mkubwa wa michezo ambaye ameshashika nafasi mbalimbali.

Kwa sasa maandalizi kwaajili ya Mkutano wa Wadau wa Majimaji FC “Wanalizombe” yanaendelea vyema na wanaohitaji taarifa wanaweza kuwasiliana na Bwana Nasib Mahinya kwa 0655 468800.

Pia viongozi wa Majimaji FC kama Katibu Mkuu Majimaji FC 0752 622887

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 30, 2013

    Ni vizuri kwa Klabu kongwe kama MajiMaji ikarudishiwa hadhi yake ya kale kwani ni kweli kwamba kuna kipindi ilikuwa ni tishio na hasa baada ya kusajili/kuchukuwa baadhi ya wachezaji nyota kutoka sehemu mbali mbali nchini.
    Si kweli kwamba klabu hiyo ilizalisha wachezaji nyota kama Abdalla Kibadeni,Peter Tino, Iddi Pazi, Omari Hussein, Mdachi Kombo na wengineo bali wachezaji waliotajwa ni baadhi ya wale ambao tayari walikuwa na majina makubwa kutoka klabu za Simba, Pan African, Yanga za bara na Navy (sasa KMKM) ya Zanzibar na kamwe hawakuinuliwa kimajina na klabu hiyo. Wangewataja wachezaji kama Samli Ayoub (beki mstaarabu) hapo ingekuwa kweli.
    Hata hivyo kwa soka la kileo nadhani klabu ifanye juhudi za makusudi kurejea historia hiyo ambayo klabu nyingine ndio zinaiga wakati MajiMaji ambao ndio waanzilishi baadae waliamua kulala fofofo na hatimaye kukaribia kufa. Kamwe timu haiwezi kujiimarisha kwa kutegemea wachezaji kutoka Songea na Mbinga tu bali ni lazima ijitanue kama ilivyokuwa miaka ile ya kale.
    Nitazipongeza sana juhudi za kuifufua hiyo timu lakini kwa kuangalia soko la mbali la wachezaji badala ya kung'ng'ania hapo Lizaboni pekee.
    Nawasilisha.
    Wenu mwanasoka mkali wa kale kutoka Makunduchi, Zanzibar.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 30, 2013

    Hii taarifa imekosewa!!Majimaji haikuzalisha wachezaji wote waliotajwa hapo juu bali iliwachukua kutoka klabu kubwa za Tanzania na walinunuiwa kwa pesa nyingi aliotoa mfadhili wao Shafii Bora...Michuzi rekebisha hilo plzz.Wachezaji waliozalishwa na Majimaji ni akina celestine Sikinde Mbunga,Octavian Mrope,Samli Ayoub na wengineo...
    Mdau wa Oxford.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 31, 2013

    Du umenikumbusha celestine sikinde mbunga mzee wa cross zinazoingia wavuni zenyewe bila kuguswa,Beckam hapo baaado hatumjui.

    ReplyDelete
  4. Mdachi Kombo alianzisha kitu kikubwa sana hapo Songea! Ligi ya vijana,ilikuwa je akafa jamani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...