Kutoka Kulia niMwenyekiti wa TEHAMA Class na Msanii wa Kizazi
Kipya Bongo Flave, Inspector Haorun aka Babu akiwa na watalaamu wa
TEHAMA(ICT) wapili ni Diana Mtambalike ambaye ni Katibu wa kampuni
hiyo,Mkurugenzi Mtendaji wa Fahamu Campany ambao ndio waandaji na
watoaji wa elimu ya TEHAMA kwa shule za msingi Bw, Mstafa Rubunda
,Mtalamu wa maswala ya TEHAMA, na Meneja wa Ufundi wa F
ahamu Campany.Yusuph Kannokole wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizaka semina ya Viongozi  ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya semina
ya wasanii zaidi ya 100.
=========   =======  =======
Kampuni ya Fahamu inayojihusisha na utoaji wa elimu Tehama( ICT) kwa
shule za msingi jijini Dar es Salaam, imeamua kuingia ndani zaidi
katika kutoa elimu kwa shule za msingi kwa kushirikiana na wasanii wa
muziki wa kizazi kipya bongo freva na wasanii wa filam nchini
.

Akizungumzia umuhimu wa utoaji wa elimu hiyo ya TEHAMA kwa shule za
msingi Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bwana Mustafa Rubunda alise ameona kuna umuhimu wa kutoa mafunzo hayo kwa watoto wa shule za msingi kuanzia darasa la pili hadi la saba hii ni kutokana na
changamoto ya mabadiliko ya kisayansi na teknolojia amba vijana hao
watakuwa na uwezo wa kiubunifu pamoja na kibiashara.


Pia alisema mafunzo hayo yatawafanya wanafunzi kujua teknolojia
nini,umuhimu wa habari,matumizi ya mawasiliano,huwa wepesii wa kuelewa na kuwa wabunifu hii itawafanya wanafunzi kuendana na mfumo wa Sayansi na Teknolojia itakayowawezesha  kuingia katika ushindani zaidi na wanafunzi wenzao wa Afrika mashariki,na Duniani kwa ujumla

  Mstafa alisema kuwa ili kuhakikisha lengo linakamiliaka Kampuni yake
ya Fahamu imeamua kuandaa semina kwa wasanii mbalimbali zaidi ya 100,
ambao wataongozwa na Msanii mkongwe Inspector Haorun aka babu,ambaye ndiye Mwenyekiti wa TEHAMA CLASS,na mwakilishi wa wasanii.


Semina hiyo inategemea kufanyika Mwezi huu jijini Dar es Salaam,
ambapo itawajumuisha wasanii ,wanafunzi wa sekondari, pamoja na wa
Vyuo Vikuu  lengo la kuwa jumuisha katika semina ni kuona umuhimu wa
kuweza kuwasaidia wadogo zao katika kuhakikisha wanakuwa watumiaji wa TEHAMA ambayo sasa ndiyo iliyobeba Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano.

 
Kulingana na uzoefu ambao tayari Fahamu Company  kutokana na kutoa
mafunzo kama hayo kwa shule za msingi za Mapinduzi na Rutihinda
zilizopo Kigogo katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam,
alisema kuwa watoto watapata fursa ya kusoma kwa bidii kwani hata
wenzao wamekuwa na morali mkubwa wa kujifunza masomo hayo.

Kwa upande wa serikali kupitia TAMISEMI, wamekuwa bega kwa bega kwa
kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Fahamu Campany kwa ajili ya kutoa
elimu hiyo kwa watoto wa shule za msigi nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 16, 2013

    Babu mtoto wa geti kali, utu uzima huo.Ila nakufagilia sana una hekima sana kijana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...