Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza katika Mkutano wa Teknolojia ya Kupambana na Uhalifu uliofanyika katika Jiji la Lyon nchini Ufaransa hivi karibuni. Waziri Nchimbi alishiriki mkutano huo pamoja na washiriki wengine kutoka nchi mbalimbali duniani.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (katikati) akimsikiliza kwa makini Rais wa Shirika la Kimataifa la Polisi (Interpol), Mireille Ballestrazzi (kushoto) baada ya Mkutano wa Kimataifa wa Teknolojia ya Kupambana na Uhalifu uliofanyika katika Jiji la Lyon nchini Ufaransa hivi karibuni. Kulia ni Meya wa jiji hilo, Gerald Collomb.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Shirika la Kimataifa la Polisi (Interpol) Mireille Ballestrazzi (kushoto) na Kulia ni Meya wa Jiji la Lyon, Gerald Collomb. Waziri Nchimbi alishiriki mkutano huo wa Kimataifa hivi karibuni. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2013

    Duh hongera mwana mama kwa kuongoza shirika kubwa kama hilo.

    Najua mutaniambia mimi ni conservative lakini ametumia juhudi za ziada kufikia hapo.

    ReplyDelete
  2. mwanamama mzuri sijui Mbrazil halafu hiyo pozi ya picha ya kwanza kwa waziri wetu inanitia wasi wasi sana Maana ufaransa kule

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...