Naitwa  Mama  Jessica, ni mwanamke mwenye  umri  wa  miaka  35, mkaazi  wa  Tabata, Dar  Es salaam.. Baada  ya  kuumizwa  sana    na  wanaume katika  mapenzi, niliamua  kutafuta  mganga wa  kienyeji, shoga  yangu  alinipeleka  kwa Mganga mmoja  anayeitwa  MUNGU  WAKABILI, ambaye  ni  Mtaalamu  aliyebobea   sana katika  masuala  ya  ULIMWENGU  USIO ONEKANA. 
Wakati naenda  kumuona  huyu  mganga, tayari  nilikuwa nimeanza  uhusiano  na  mwanaume mmoja lakini  na  yeye  akawa   haeleweki  heleweki. MUNGU  WAKABILI, alinipa  dawa   ya  mapenzi   ambayo  imenifanya  nijutie   kuitumia , kwani  baada  ya  kumfanyia  dawa  mwanaume  huyo, AMENIPENDA   KUPITA  KIASI! YANI AMEKUWA  KAMA   ZEZETA  KABISA! 
Alikuwa  na  mke  wa  ndoa na  watoto  watatu, ila amewatelekeza  wote   na  kuja  kuishi  na  mimi. Nyumba  aliyo jenga  na  mke  wake  ameiuza  na  kuninunulia  mimi  nyumba  nyingine   ili  tuishi  pamoja, kama  hiyo  haitoshi  alikuwa  na  magari  mawili  moja  amempa  mdogo  wangu  wa  kiume, jingine  ameliuza  na kunifungulia  duka  la  nguo  Kinondoni.   Ni mambo mengi  sana, yote  siwezi  kuelezea, ila kibaya  zaidi  ni kwamba, sasa  ameshindwa  kuendelea  na  biashara  zake,anataka  kuwa  na  mimi  wakati  wote  kwa  sababu  amekuwa  na  wivu  sana, anahisi akiniacha  hata  kwa  dakika  mbili tu nitaibiwa  na  mwanaume mwingine. Kibaya  kuliko  vyote  sasa  ndugu  wa  mume, mke  wake  na  ndugu  wa  mke wake, wameanza  kunitishia  maisha  yangu . 
Nilijaribu  kwenda  kumuomba  huyu MUNGU  WA  KABILI  anipe  dawa  ya  kumrudisha  huyu mwanaume  katika  hali  yake  ya  kawaida  lakini  amegoma  kufanya  hivyo, anasema yeye   hawezi  kuharibu dawa  aliyo kwisha  itengeneza tayari  na  kwamba  alinionya  mapema.. Hapa  nipo njia  panda  na  sijui  hatma  ya jambo  hili, natamani  nikimbie  mji  lakini  nashindwa.  
Nimeamua  kuandika  waraka huu  ili  kwanza, kuwaonya  wanawake  wenzangu  waachane  na   MAPENZI  YA  KICHAWI  ili  yasije  kuwakuta  kama  yaliyo nikuta  mimi, kwani naona  wanawake  wengi sana, wa  Dar  Es salaam, wanamkibilia  mtu  huyu  kwa  ajili  ya  kupata  dawa  za  mapenzi.. 
Nakuonya  usifanye  hivyo mwanamke  mwenzangu, kwani  mtu  huyu  licha  ya  kuwa  na  umri  mdogo  tu tena  wa  miaka  chini  ya  thelathini, lakini  dawa  zake  ni  za  hatari  sana  na  zina  nguvu  za  ajabu  sana! Usijaribu  kabisa  mwanamke  mwenzangu,  utaumbuka,kwani kila  mtu  atajua  umetumia  uchawi!  
 Lakini, pili, ninawaomba  wanawake  wenzangu  mnisaidie   kumshawishi     MUNGU  WA KABILI  ili  amrejeshe  huyu  mwanaume  katika  hali  yake  ya  kawaida.. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. Hello Jessca,this is good news for me.Tafadhali sana sana nakuomba unipatie namba ya simu ya huyu mungu please,ninamatatizo makubwa sana.mdau UNITED STATE.

    ReplyDelete
  2. hakuna kitu kama hicho, itabidi uendelee tu na mumwe wako;

    ReplyDelete
  3. Hili ni tangazo la biashara au?

    ReplyDelete
  4. nenda kanisa lililo karibu yako ukamueleza mchungaji au padre nae atakuongoza sala ya toba. hiyo tu itatosha

    ReplyDelete
  5. naomba unielekeze kwa "MUNGU WAKABILI" nami nkachukue ya kwangu tafadhari

    ReplyDelete
  6. Naomba serikali imkamate haraka sn huyu mwanamke kisha awaonyeshe alipo huyu mshenzi MUNGU WAKABILI iliafungwe maisha jela,na huyu MAMA JESSICA pia,kwakweli huu ni ushetani baba wa watu kageuzwa kuwa ZEZETA hii hatali sn ndugu zangu watanzania haya mambo ci ya kufumbia macho,kumbe tunaowaona mitaani wamelazimishwa UZEZETA inauuuma saaaana,poleni sn wenye huyu ndugu aliepewa uzezeta kwamakusudi,

    ReplyDelete
  7. nipe hiyo contact ya huyu mganga na mimi nna wangu

    ReplyDelete
  8. Kwanza unastahili sifa kwa ujasiri na consideration na pia unastahili lawama. Swali; unasema kuwa unajuta je kwa nini ulitafuta mganga wakati huyu jamaa hakuwa miongoni mwa hao wanaume unaodai wamekuumiza kimapenzi? Je lengo hapa ilikuwa ni nini wakati ulifahamu wazi kuwa huyo jamaa alikuwa na mke wake? Je unafikiria ni nani wa kulaumiwa khapa kati ya mganga ana wewe. Kwa hiyo fanya jambo la msingi; rudisha vitu vyote alivyokupa, yaani rudisha nusu hasara kwa mkewe kama wewe kweli unajutia hayo. Tafuta japo mtu arejeshe kwa niaba yako. Au unatuchezea akili isije kuwa hili ni tangazo la biashara la mganga?

    ReplyDelete
  9. wewe dada uliyoleta hii habari unajua tunaye Mungu mmoja tu aliyetuuma ana kaumba vyote dunia nzima ni yeye anamamlaka yote kwa nini unaabudu waganga waliubwa kama wewe kwanza umefanya kosa kubwa sana kwenda kwa waganga mganga ni nani tuna mganga mmoja tu naye Munga Baba aliyetuumba mrudie muumba wako ukatubu mimi sijui wewe ni dini gani lakini kama ni mkiristo nenda kwa mchunga wako mweleze madhambi yako utubu na akuombee wacha kabisa hili neno lakusema watu wakamwombe huyu mganga alegeze masharti kitu kitakacho kusaidii wachan kabisa na huyu mganga mjeukie muumba wako hakuna lisilowezekana kwake na ukimwomba kwa dhati na kutubu madhambi yako atasikia sala zako na kukusamehe na kukusaidia kuliko kumtumainia mwanadamu kama wewe mimi ni hayo tu ukipenda fuata usipopenda wacha ni uwamuzi wako

    ReplyDelete
  10. mie naona kama unampigia chepuo huyo mganga, mwanamke gani asiyetaka kununuliwa gari, nyumba, kufunguliwa biashara na kupendwa?

    ReplyDelete
  11. Ndoa ya mwanamke mwenzako uliyoivunja laana itaambatana nawe hadi kizazi cha 4! nenda madhabauni ungaungame na sio kulalama @#$%^@!& Mkubwa wewe! EBO!

    ReplyDelete
  12. Mshawasha wa kumrudisha kwa mumewe unao wewe au nitafute nikupatie.
    nipigie 078 421 1726

    ReplyDelete
  13. Tafuta hela (unazo kwa jinsi zezeta alivyowekeza kwako) na nendeni wote nyie wawili kwa TB Joshua, atafanya vitu vyake mtakuwa huru. Lakini sasa mumewe huyo atarudi kwa mke wake wa ndoa......utajiju!!

    ReplyDelete
  14. hahaha hata mm nahitaji contact za huyo mganga wanaume viburi sana na huyu mnganga ndo dawa yao

    ReplyDelete


  15. Uongo mtupu, hamna kitu kama hicho, huyu anatuchezea akili tu.

    ReplyDelete
  16. HII IMEKAA ZAIDI KAMA TANGAZO LA BIASHARA NA SIYO KUTOA USHAURI

    ReplyDelete
  17. Hili liwe fundisho kwa wanaume wanaotongoza tongoza hovyo, sasa huyu ni kitu gani kilimpeleka kutongoza mke mwingine wakati ana mke wake na watoto ?

    ReplyDelete
  18. Kwanza, Pole sana. Nenda mbele za Mungu ukiri ukimaanisha kwa moyo wa dhati na Mungu atakusikia. Fanya hivyo haraka umrudishie akili zake baba wa watu na uachane na hiyo dhambi.

    Pili, Naomba contact za mganga huyu nimpe wifiangu nae akaroge maana ameshahangaika sana kwa waganga kupata dawa ya mapenzi hajafanikiwa teh teh teh, kaaazi kweli kweli

    ReplyDelete
  19. Duh! Promo la nguvu. Sidanganyiki lakini.

    ReplyDelete
  20. msemakweliAugust 20, 2013

    Promo ya nguvu kwa huyu 'mganga' hakuna lolote uzushi mtupu. Mjini kweli shule.n

    ReplyDelete
  21. KAMA HUYO MGANGA WAKO ANAYO DAWA YA MIMI KUINGIZA BEGI 20 ZA SEMBE MAREKANI NIUNGANISHE NAE CHONDE CHONDE DADA YANGU ...LOL

    ReplyDelete
  22. kwa kweli wadau hata mimi linaniingia akilini kuwa hili ni tangazo na aliyeposti ni huyo mganga mwenyewe.teh teh....

    ReplyDelete
  23. Sifikiri kama huyu msichana katumia dawa yeyote ya mapenzi. Nionavyo mimi ni kijana huyu bila shaka amebarikiwa ya silaha kali, na hilo jamaa limegeuzwa kuwa zombi kwa matumizi ya silaha siyo dawa.

    ReplyDelete
  24. Duu kweli ndio maana watu wanasoma marketing miaka mitatu au minne chuo kikuu unafikiri wanacheza! Ndio kazi yao hiyo! Chezea elimu!

    ReplyDelete
  25. Naungana na mdau aliyesema anampigia chepuo huyo mganga na si kwamba anasikitika. hapa ki-msingi anatangaza biashara in a negative way

    ReplyDelete
  26. Acheni kudanganyika munaotaka contact za mganga mtapoteza hela zenu bure, Mganga ni YESU peke yake ndiye anayeweza kumfunga mume wako asiruke na vicheche.

    ReplyDelete
  27. Hahahahaha,aii,hovyoooo! tangazo la biashara hili

    ReplyDelete
  28. Upumbavu mtupu sijuwi kwa nini nimesoma upuuzi huu.

    ReplyDelete
  29. Mganga wa Kieyeji huyo anatoa tangazo la Biashara kwa dizaini yake. OGOPA TAPELI! CHEZEA BONGO WEYE?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...