Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara akimkabidhi Tuzo ya Ben TV Diplomatic Awards-2012 Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ofisini kwake tarehe 19.8.2013. Tuzo hiyo ilitolewa kwa Mama Salma baada ya kuibuka mshindi miongoni mwa mataifa ya bara la Afrika, Caribean, Asia na Pacific kutokana na kazi za kuendeleza rasilimai watu hapa Tanzania.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akitoa hotuba fupi ya kushukuru mara tu baada ya kupokea Tuzo kutoka kwa Taasisi ya Bright Entertainment Network ya Uingereza iliyokabidhiwa kwake na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara tarehe 19.8.2013.
Mwnyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akipiga picha ya pamoja na Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo mara baada ya Waziri Mukangara kumkabidhi Tuzo hiyo.
Mke wa Rais na Mshindi wa Tuzo ya BEN TV DIPLOMATIC AWARDS-2012 Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara na baadhi ya wajumbe wa bodi ya WAMA, Mheshimiwa Zakhia Meghji, Makamu Mwenyekiti (kulia) na Mama Hulda Kibacha, Mjumbe wa bodi (kushoto).mara tu baada ya kupokea Tuzo hiyo ofisini kwake tarehe 19.8.2013.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akimsikiliza kwa makini Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt.Fenella Mukangara wakati akitoa maelezo mafupi kuhusiana na tuzo ya Ben TV Diplomatic Awards-2012 aliyopewa dhamana na Taasisi ya Bright Entertainment Network (BEN) ya Uingereza ya kumkabidhi Mama Salma Kikwete Tuzo hiyo katika jitihada zake za kuendeleza rasilimali watu katika Taifa kwa mwaka 2012.PICHA NA JOHN LUKUWI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Dkt. Fenella suka yake ni safi sana yaani wa mama wangefuata mfano wake badala ya kuvaaa manyelwe ya bandia na huu ndiyo Uafrika halisi. Naona na midume ndiyo imeanza kusuka namna hii sijui ndiyo ushoga.

    ReplyDelete
  2. Keli kabisa mdau hapo juu, huyu mama Dkt. Fenella na mkubali sana. Nashindwaga kuelewa kwanini waafrika hatujikubali? Yani muda tunao poteza kujilemba na mawigi na nywele bandia ni mwingi sana.
    Embu mama na dada zetu badilikeni, kuweni waafrika halisi sio kutukuza uzungu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...