Naitwa Mama Jessica, ni mwanamke mwenye umri wa miaka 35, mkaazi wa Tabata, Dar Es salaam.. Baada ya kuumizwa sana na wanaume katika mapenzi, niliamua kutafuta mganga wa kienyeji, shoga yangu alinipeleka kwa Mganga mmoja anayeitwa MUNGU WAKABILI, ambaye ni Mtaalamu aliyebobea sana katika masuala ya ULIMWENGU USIO ONEKANA.
Wakati naenda kumuona huyu mganga, tayari nilikuwa nimeanza uhusiano na mwanaume mmoja lakini na yeye akawa haeleweki heleweki. MUNGU WAKABILI, alinipa dawa ya mapenzi ambayo imenifanya nijutie kuitumia , kwani baada ya kumfanyia dawa mwanaume huyo, AMENIPENDA KUPITA KIASI! YANI AMEKUWA KAMA ZEZETA KABISA!
Alikuwa na mke wa ndoa na watoto watatu, ila amewatelekeza wote na kuja kuishi na mimi. Nyumba aliyo jenga na mke wake ameiuza na kuninunulia mimi nyumba nyingine ili tuishi pamoja, kama hiyo haitoshi alikuwa na magari mawili moja amempa mdogo wangu wa kiume, jingine ameliuza na kunifungulia duka la nguo Kinondoni. Ni mambo mengi sana, yote siwezi kuelezea, ila kibaya zaidi ni kwamba, sasa ameshindwa kuendelea na biashara zake,anataka kuwa na mimi wakati wote kwa sababu amekuwa na wivu sana, anahisi akiniacha hata kwa dakika mbili tu nitaibiwa na mwanaume mwingine. Kibaya kuliko vyote sasa ndugu wa mume, mke wake na ndugu wa mke wake, wameanza kunitishia maisha yangu .
Nilijaribu kwenda kumuomba huyu MUNGU WA KABILI anipe dawa ya kumrudisha huyu mwanaume katika hali yake ya kawaida lakini amegoma kufanya hivyo, anasema yeye hawezi kuharibu dawa aliyo kwisha itengeneza tayari na kwamba alinionya mapema.. Hapa nipo njia panda na sijui hatma ya jambo hili, natamani nikimbie mji lakini nashindwa.
Nimeamua kuandika waraka huu ili kwanza, kuwaonya wanawake wenzangu waachane na MAPENZI YA KICHAWI ili yasije kuwakuta kama yaliyo nikuta mimi, kwani naona wanawake wengi sana, wa Dar Es salaam, wanamkibilia mtu huyu kwa ajili ya kupata dawa za mapenzi..
Nakuonya usifanye hivyo mwanamke mwenzangu, kwani mtu huyu licha ya kuwa na umri mdogo tu tena wa miaka chini ya thelathini, lakini dawa zake ni za hatari sana na zina nguvu za ajabu sana! Usijaribu kabisa mwanamke mwenzangu, utaumbuka,kwani kila mtu atajua umetumia uchawi!
Lakini, pili, ninawaomba wanawake wenzangu mnisaidie kumshawishi MUNGU WA KABILI ili amrejeshe huyu mwanaume katika hali yake ya kawaida..
Hello Jessca,this is good news for me.Tafadhali sana sana nakuomba unipatie namba ya simu ya huyu mungu please,ninamatatizo makubwa sana.mdau UNITED STATE.
ReplyDeletehakuna kitu kama hicho, itabidi uendelee tu na mumwe wako;
ReplyDeleteHili ni tangazo la biashara au?
ReplyDeletenenda kanisa lililo karibu yako ukamueleza mchungaji au padre nae atakuongoza sala ya toba. hiyo tu itatosha
ReplyDeletenaomba unielekeze kwa "MUNGU WAKABILI" nami nkachukue ya kwangu tafadhari
ReplyDeleteNaomba serikali imkamate haraka sn huyu mwanamke kisha awaonyeshe alipo huyu mshenzi MUNGU WAKABILI iliafungwe maisha jela,na huyu MAMA JESSICA pia,kwakweli huu ni ushetani baba wa watu kageuzwa kuwa ZEZETA hii hatali sn ndugu zangu watanzania haya mambo ci ya kufumbia macho,kumbe tunaowaona mitaani wamelazimishwa UZEZETA inauuuma saaaana,poleni sn wenye huyu ndugu aliepewa uzezeta kwamakusudi,
ReplyDeletenipe hiyo contact ya huyu mganga na mimi nna wangu
ReplyDeleteKwanza unastahili sifa kwa ujasiri na consideration na pia unastahili lawama. Swali; unasema kuwa unajuta je kwa nini ulitafuta mganga wakati huyu jamaa hakuwa miongoni mwa hao wanaume unaodai wamekuumiza kimapenzi? Je lengo hapa ilikuwa ni nini wakati ulifahamu wazi kuwa huyo jamaa alikuwa na mke wake? Je unafikiria ni nani wa kulaumiwa khapa kati ya mganga ana wewe. Kwa hiyo fanya jambo la msingi; rudisha vitu vyote alivyokupa, yaani rudisha nusu hasara kwa mkewe kama wewe kweli unajutia hayo. Tafuta japo mtu arejeshe kwa niaba yako. Au unatuchezea akili isije kuwa hili ni tangazo la biashara la mganga?
ReplyDeletewewe dada uliyoleta hii habari unajua tunaye Mungu mmoja tu aliyetuuma ana kaumba vyote dunia nzima ni yeye anamamlaka yote kwa nini unaabudu waganga waliubwa kama wewe kwanza umefanya kosa kubwa sana kwenda kwa waganga mganga ni nani tuna mganga mmoja tu naye Munga Baba aliyetuumba mrudie muumba wako ukatubu mimi sijui wewe ni dini gani lakini kama ni mkiristo nenda kwa mchunga wako mweleze madhambi yako utubu na akuombee wacha kabisa hili neno lakusema watu wakamwombe huyu mganga alegeze masharti kitu kitakacho kusaidii wachan kabisa na huyu mganga mjeukie muumba wako hakuna lisilowezekana kwake na ukimwomba kwa dhati na kutubu madhambi yako atasikia sala zako na kukusamehe na kukusaidia kuliko kumtumainia mwanadamu kama wewe mimi ni hayo tu ukipenda fuata usipopenda wacha ni uwamuzi wako
ReplyDeletemie naona kama unampigia chepuo huyo mganga, mwanamke gani asiyetaka kununuliwa gari, nyumba, kufunguliwa biashara na kupendwa?
ReplyDeleteNdoa ya mwanamke mwenzako uliyoivunja laana itaambatana nawe hadi kizazi cha 4! nenda madhabauni ungaungame na sio kulalama @#$%^@!& Mkubwa wewe! EBO!
ReplyDeleteMshawasha wa kumrudisha kwa mumewe unao wewe au nitafute nikupatie.
ReplyDeletenipigie 078 421 1726
Tafuta hela (unazo kwa jinsi zezeta alivyowekeza kwako) na nendeni wote nyie wawili kwa TB Joshua, atafanya vitu vyake mtakuwa huru. Lakini sasa mumewe huyo atarudi kwa mke wake wa ndoa......utajiju!!
ReplyDeletehahaha hata mm nahitaji contact za huyo mganga wanaume viburi sana na huyu mnganga ndo dawa yao
ReplyDelete
ReplyDeleteUongo mtupu, hamna kitu kama hicho, huyu anatuchezea akili tu.
HII IMEKAA ZAIDI KAMA TANGAZO LA BIASHARA NA SIYO KUTOA USHAURI
ReplyDeleteHili liwe fundisho kwa wanaume wanaotongoza tongoza hovyo, sasa huyu ni kitu gani kilimpeleka kutongoza mke mwingine wakati ana mke wake na watoto ?
ReplyDeleteKwanza, Pole sana. Nenda mbele za Mungu ukiri ukimaanisha kwa moyo wa dhati na Mungu atakusikia. Fanya hivyo haraka umrudishie akili zake baba wa watu na uachane na hiyo dhambi.
ReplyDeletePili, Naomba contact za mganga huyu nimpe wifiangu nae akaroge maana ameshahangaika sana kwa waganga kupata dawa ya mapenzi hajafanikiwa teh teh teh, kaaazi kweli kweli
Duh! Promo la nguvu. Sidanganyiki lakini.
ReplyDeletePromo ya nguvu kwa huyu 'mganga' hakuna lolote uzushi mtupu. Mjini kweli shule.n
ReplyDeleteKAMA HUYO MGANGA WAKO ANAYO DAWA YA MIMI KUINGIZA BEGI 20 ZA SEMBE MAREKANI NIUNGANISHE NAE CHONDE CHONDE DADA YANGU ...LOL
ReplyDeletekwa kweli wadau hata mimi linaniingia akilini kuwa hili ni tangazo na aliyeposti ni huyo mganga mwenyewe.teh teh....
ReplyDeleteSifikiri kama huyu msichana katumia dawa yeyote ya mapenzi. Nionavyo mimi ni kijana huyu bila shaka amebarikiwa ya silaha kali, na hilo jamaa limegeuzwa kuwa zombi kwa matumizi ya silaha siyo dawa.
ReplyDeleteDuu kweli ndio maana watu wanasoma marketing miaka mitatu au minne chuo kikuu unafikiri wanacheza! Ndio kazi yao hiyo! Chezea elimu!
ReplyDeleteNaungana na mdau aliyesema anampigia chepuo huyo mganga na si kwamba anasikitika. hapa ki-msingi anatangaza biashara in a negative way
ReplyDeleteAcheni kudanganyika munaotaka contact za mganga mtapoteza hela zenu bure, Mganga ni YESU peke yake ndiye anayeweza kumfunga mume wako asiruke na vicheche.
ReplyDeleteHahahahaha,aii,hovyoooo! tangazo la biashara hili
ReplyDeleteUpumbavu mtupu sijuwi kwa nini nimesoma upuuzi huu.
ReplyDeleteMganga wa Kieyeji huyo anatoa tangazo la Biashara kwa dizaini yake. OGOPA TAPELI! CHEZEA BONGO WEYE?
ReplyDelete