Nafurahi kuona maoni mbali mbali ya wadau tofauti. Kila mmoja amezungumza kwa kuzingatia maslahi ya Taifa letu. Kikubwa naomba tutofautishe uraia wa nchi mbili kwa Mtanzania mzaliwa(Maganga) VS mgeni kupata uraia wetu(Rajper).
Maganga yeye hana shida kabisa, kwasababu uraia wake wa kuzaliwa atabaki nao, kazi kwake kuupata wa nchi nyingine kwa kufuata masharti ya hiyo nchi. Kama ni USA, basi afuate utaratibu wake lakini asipoteze uraia wa Tanzania.
Nadhaani wachangia mada hakuna anayemkataa Maganga kubaki na uraia wake. Sasa twende kwa Rajper, yeye anautaka uraia wetu, lazima afuate masharti yetu (magumu) kabla ya kuuchukua. Mfano kuna kitu kinaitwa birth rights ambavyo hata huku ughaibuni tunakumbana navyo.
Kwa nchi yetu, kutokana na umaskini wetu, lazima tuwe makini kabisa. Birth rights aliyonayo Maganga asipewe Rajper. Maganga aruhusiwe kugombea nafasi za uongozi kisiasa, Rajper hapana. Mtoto wa Maganga apewe nafasi ya kuchagua once anapotimiza 20 years kati ya birth rights za TZ au za huko alikozaliwa. Bado anaruhusiwa kuwa na uraia wa nchi mbili,lakini birth right achague.
Rajper akipata watoto ndani ya ardhi ya Tanzania,na mmoja wa mzazi ni Mtanzania, basi huyo ni mwenzetu, apewe birth rights.
Vitu kama investments, lazima brith right ifanye kazi, mwekezaji lazima atoe % kwa mzawa ili kulinda raslimali zetu. Kama ni madini,basi Rajper asiruhusiwe 100% kuinvest mwenyewe,lazima kuwe na mzalendo. Akijenga nyumba, basi anakodishiwa ardhi, lakini Maganga akijenga nyumba ni yake na ardhi ni yake.
List ni ndefu,lakini lazima tutofautishe uraia wetu na Birth rights" ambazo laziwe zitajwe kwenye katiba.
Mungu ibariki TZ, Mungu ibariki Africa
Ubarikiwe kwa mawazo mazuri kwa misingi hiyo mimi binafsi nakubali, umenishawishi kuwa uraia wa nchi unawezekana ila ufanyike kwa makini.
ReplyDeleteHoja yako poa sana na inaelimisha. Ulischokiandika ndicho mataifa mengine yanafanya. Maganga anapopewa uraia wa USA anakuwa ni "naturalized citizen" Kisheria, haruhusiwi kugombea urais USA. Unapomfutia uraia wake wa Tanzania wa kuzaliwa "citizen by birth" maaana yake unamnyima haki ya kugombea urais duniani. Huo ni mfano mmoja tu katika mifano zaidi ya elfu moja. Manganga anapoomba "American naturalized citizenship" hana maana ya kuuchukia his Tanzanian "citizenship by birth", bali anajaribu kupata maslahi mazuri USA ambayo masharti yake ni lazima awe rai wa USA ili kujaribu kuwakomboa wana ukoo wake pale Buhangija. Anapokuja Snowden toka USA kuomba uraiwa Tanzania na kutimiza masharti yetu ya kutisha, tumpatie "Tanzanian naturalized citizenship" na obvious atabaki na his "American citizenship by birth" Na kwavile USA haimruhusu Maganga kugombea urais USA, basi Tanzania isimruhusu Snowden kugombea hata ukatibu kata. Hicho ndichi kilio cha watz wanaishi diaspora. Wale watz wenzangu mnaonipinga kwa kisingizio cha kuhatarisha usalama, naomba hoja kuwa Maganga atahatarisha vipi usalama wa nchi? Tanzania atarudi na atazikwa Buhangija. Hilo halina ubishi.
ReplyDeleteMawazo mazuri sana,maana wengi wanakataa watanzania walio nje kupewa raia mbili ila wanakubali wageni wanaokuja tanzania kuwa na uraia wa nchi mbili, aliyozaliwa na hapo anapoishi now ,TZ.
ReplyDeleteWazungu ,wahindi ,na wengineo waliozaliwa nje wote bado wanauraia wao wa walikotoka ila sisi wabongo ndio hatuna.
Hakika kaka, huo ndio ukweli,mie sina cha kuongeza,
ReplyDeleteMungu ibarik tz,
mungu Ibaraki afrc.
Mdau japan.
mawazo mazuri sana, simple and very clear to understand. Inatia moyo sana kuona watu wanamawazo mazuri namna hii.
ReplyDeleteasante
Mdau UK
Safi mdau. Sikuwahi kufikiria issue ya birth rights
ReplyDeleteUraia wa nchi mbili hauepukiki katika dunia ya sasa; suala ni umakini tu...
ReplyDeletehakuna mambo ya uraia wa nchi mbili sasa baadae itakuwa wa nchi tatu, sasa hivi ninyi watanzania kweli akili tunazo? mtu awe mmarekani halafu awe mtanzania kweli kitu hicho kina leta sence? mimi sikubali kama wewe mtanzania uwe mtanzania ukibadili kuwa mmarekani basi uwe mmarekani sio huku na huku na nyie mmekuwa kina nani hasa! kuwa raia ina maana una haki zote hata urais unaweza gombania, sasa ugombanie marekani, ukishindwa uje ugombanie tanzania kweli hio ni akili?.
ReplyDeletewewe unakuwa mtanzania mwenye uraia wa sweden umekuja bongo umekorofisha hukubongo tunanyonga kawaida kama mauaji , na sweden hawaui ina maana utaomba serekali ya sweden wakuombee ukafungwe huko kwa sababu huwezi kunyongwa?
ACHENI ULIMBUKENI WENU KAMA BOX LIMEKUSHINDENI FANYENI MRUDI BONGO! SIO KULETA LETA MAMBO AMBAYO SIO YA KAWAIDA NA NINAIOMBA SEREKALI ISIKUBALI KABISA NA MAWAZO HAYA KWA WATU WALIOCHOKA NA MAISHA. KWANZA KITU GANI MAKUJA WEKEZA HUKU? WOTE HAMNA UWEZO WA KUWEKEZA NI MANENO TU YAKUNYWA BEER VIJIWENI MNAKUWA KAMA MMEPAGAWA
uafrika bwana ni kitu cha roho mbaya wakati wote, usa wanaruhusu kuwa na uraia 2 na ni nchi 11 tu kama usa dunia nzima, sasa wewe ni mtanzania na lazima uukane ili upate uraia tuseme ujerumani, itakuwaje??? maisha sio rahisi na kwa mistari 2 kama mnavyofikiria nyie wabongo!!
ReplyDeleteHiyo nakubaliana maganga kuwa na haki zaidi. Lakini katiba ya Kenya inatoa uwezo wa raia kama Maganga kupata uraia wa nchi yake na wa nchi nyingine lakini haimruhusu Maganga wala Rajper kugombea nafasi yoyote ya serikali (State officer/public official). Marekani rais lazima awe mzaliwa wa huko.Kwa sababu ya issues za kuwa na allegiance mbili Maganga na Rajper lazima wakubali kukosa haki zingine kama za kututawala kwa mfano.
ReplyDeleteJamani watanzania twende na wakati. Tuache roho mbaya na wivu, kama nchi zote za Afrika Mashariki wameshakubali kwanini sisi iwe tatizo kubwa? Watanzania wote walio nje wakimiminika Bongo watafanya kazi gani? Mbona wengi tu wako Bongo hawana kazi? Watu wanatafuta maisha sio kama hawana uzalendo au kua hawapendi nchi yao. Jamani roho ya korosho tuache la sivyo kila siku tutakua nyuma.
ReplyDeleteNi vizuri nchi yetu akiruhusu urai wa nchi mbili kwa wazawa walioko ughaibuni. Mfano uk hata kama umepata Uraia bado ile hali ya kabaguliwa ipo hivi karibuni nilikuwa naangalia application form ya kampuni moja kuna kipengele swali la uraia wako baadaye kuna kipengele umezaliwa wapi? Sasa Mtanzania anapochukua uraia wa Uk
ReplyDeletehakubaliki kama wazawa na huku kapoteza uraia wake wa Tanzania.
Mh: Membe alifikiri na kufanya utafiti kabla ya kuwasilisha hoja yake. Hongera Mh; we need more people like you. God Blss TZ. No politics just economics
ReplyDelete