Spika wa Bunge la Afrika Mashariki(EALA)akimsikiliza Mbunge wa bunge hilo kutoka Tanzania, Mhe Shyrose Bhanji wakati wakielekea bungeni.
Chemba ya Bunge la Afrika Mashariki inavyoonekana wakati kikao kikiendelea
Wabunge wa Tanzania kwenye bunge la Afrika Mashariki(EALA)wakitoka ndani ya ukumbi wa bunge hilo leo kupinga wabunge wenzao wanaoshinikiza hoja zao kwa kutoka kwenye vikao vya bunge. Kutoka kushoto ni Mh.Twaha Taslima,Mh.Shyrose Bhanji,Mh.Abdullah Mwinyi na Mhe Nderakindo Kessy
Mbunge wa Tanzania kwenye bunge la Afrika Mashariki(EALA) Mhe Abdullah Mwinyi akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari baada ya kutoka nje na kikao kuhairishwa hadi kesho
Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe Ali Mzee (kulia)akizungumza na wabunge wa Tanzania kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki(EALA)kutoka kushoto ni Mh.Shyrose Bhanji,Mh.Nderakindo Kessy,Mh.Twaha Taslima na Mh. Abdullah Mwinyi.
Kwa habari kamili tembelea Mwananchi: BOFYA HAPA
Kwa habari kamili tembelea Mwananchi: BOFYA HAPA
R.I.P EAST AFRICA COMMUNITY
ReplyDeleteMapema sana kulionekana na namna ya EAC kutokufanikiwa kwani nchi zingine ukiachilia mbali Tz zinajipendelea sana. Ndio maana mwalimu Nyerere aliona isiwe tabu ngoja tubaki wenyewe kwanza.
ReplyDeleteBado viongozi wetu wa sasa wanabidi kuchukua maamuzi magumu kwani hata kama jumuia ya ulaya ndio inasaidia EAC kujiendesha hakuna maana kubakia hapo. Tz tubakie wenyewe kwani juzi tu walikuwa na mkutano Uganda bila Raisi wetu, aujapita muda wamezindua bandari huko Kenya bila kumwalika Raisi wetu bado waTz tunakomaa nao? Hapana kabisa!
amen
ReplyDeleteBiashara za soko la Afrika Mashariki na ushindani ndani ya jumuia ukoje?. Hivi nchi inaweza kuvuta zingine kwenye mshikamano tofauti ili inufaike, baada ya kuona jirani amejipanga na anakuja juu?. Sio wivu ni kutaka kuelewa jumuia inaelekea wapi.
ReplyDeletekwakweli kuna haja ya kuangalia nia na madhumuni ya wenzetu wanaonekana si watu wa umoja hata kidogo. Mbona mabo mengi wanafanya kivyao vyao tu.
ReplyDeleteMwanzo mataifa yote yali lianza vizuri sana kushabikia EAC lakini sasa naona wamegundua watanzania wameshatambua nia ya baadhi ya washiriki wetu ndo maana wanaenda kwa wasio jitambua.
Naona kuna mataifa yanaangalia maslahi yao kwanza.
Binafsi naona wakati wa sisi kuungana na hao wenzetu bado saana, kwani hao umoja hawauwezi kabisa. Hebu angalia sasa hivi hata amani kati ya nchi zetu inalegalega. Mwalimu Nyerere aliona mbali!! aliona hata mambo ya miaka 10 ijayo. Hebu tutafakari kwanza kabla jua halijatua. EAC ni nzuri lakini mmh sijui. wadau toeni maoni jamani.
ReplyDelete