Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Zitto Kabwe (Mb) akionesha Leseni mpya za Udereva mbele ya wajumbe wa kamati yake wakati kamati hiyo ilipokutana na Hazina kujadili namna bora ya kukusanya mapato ya Serikali hususani yale ya makosa ya barabarani kwa kutumia mfumo wa risiti za ki electroniki kwa kuwa leseni hizo zipo kwenye mfumo wa kisasa. Kamati hiyo imeileza Hazina jinsi fedha nyingi za makusanyo mbalimbali zinavyopotea kwa kutumia mfumo wa zamani wa risiti za kawaida na hata mara nyingine serikali kutofaidika na mapato hayo licha ya kwekeza zaidi katika mifumo hii.
Mjumbe wa kamati ya Bunge ya PAC Mhe. Gaudensi Kayombo akifafanua jambo mbele ya watendaji wa Hazina wakati wakikao na Kamati hiyo.
Naibu katibu Mkuu Hazina Bi. Elizabeth Nyambibo akijibu baadhi ya hoja zilizotolewa na wajumbe wa kamati ya Bunge ya PAC kujadili masalwa mbalimbali ya utendaji wa wizara hiyo walipokutana na kamati hiyo leo.
Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali LAAC Mhe.Rajaab Mbarouk Mohamed akiongoza kikao cha kamati hiyo leo ilipokutana kujadili Hesabu za Manispaa ya Arusha wakati wa Vikao vya Kamati vinavyoendelea Jijini Dar Es Salaam. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Seleman Zedi.
Wajumbe wa Kamati ya LAAC wakifuatilia kikao kwa makini.
Mjumbe wa Kamati ya LAAC Mhe. Yusufu Nasir akiuliza swali kwa watendaji wa Manispaa ya Arusha wakati wa vikao vya Kamati ya Bunge ya LAAC jijini Dar leo. Picha zote na Owen Mwandumbya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. SAFI SANA LAKINI NAONA TUMESAHAU JAMBO MOJA MUHIMU SANA!KUPUNGUZA UZITO WA MWILI,KINAMAMA JAMANI AIBU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...