WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mhe George Mkuchika (kulia) akimpongeza Mhe Yohana Miwa kwa kuteuliwa kuwa Katibu Tawala wa wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara 
---------------------------------
Habari na picha na Abdulaziz video
 Serikali ya Wilaya ya Masasi mkoa wa Mtwara, imesema kuwa uongozi wa wilaya utahakikisha unaanza kushirikisha makundi ya watu wenye ulemavu katika shughuli mbalimbali za maendeleo kwa asilimia 100 ikiwemo kushiriki kwenye ziara za viongozi wa kitaifa wanaokwenda Wilayani humo jambo ambao litasaidia kuondoa dhana ya kunyanyapaliwa. 
Kauli hiyo imeitolewa Jumamosi na Mhe Yahana Miwa, Katibu Tawala wa wilaya hiyo,  alipokuwa akifungua mafunzo ya mkataba wa umoja wa mataifa (UN) kwa niaba ya mkuu wa Wilaya hiyo, Farida Mgomi.
Mafunzo hayo ya siku tatu yanahusu sheria na sera kwa watu wenye ulemavu mkoani Mtwara na kuandaliwa na shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu (SHIVYAWATA) mkoani humo na kufanyika katika ukumbi wa mami mjini hapa. 
Mhe Miwa alisema serikali itahakikisha kwamba makundi yote ya watu wenye ulemavu yaliyopo Masasi yanashiriki kikamilifu masuala mbalimbali ya maendeleo ili kuyapa fursa kwa makundi hayo kuweza kutoa mchango wao katika mambo ya maendeleo yanayofanyika Wilayani humo kama makundi mengine ya kijamii yanavyoshirikishwa. 
Alisema walemavu ni sawa na watu wasio walemavu hivyo wana haki ya kushiriki katika masuala mbalimbali ya maendeleo yanayofanyika katika maeneo yaliyowazunguka hivyo kuanzia serikali Wilayani Masasi inaahidi kuanza kushirikiana na makundi ya watu wenye ulemavu bega kwa bega ili kwa pamoja kuweza kuleta maendeleo Wilayani humo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. ni jambo la busara kwa mh YOHANA MIWAkuwashirikisha na kuwafanya wao wajione ,uwa ni sehemiu ya jamii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...