WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mhe George Mkuchika (kulia) akimpongeza Mhe Yohana Miwa kwa kuteuliwa kuwa Katibu
Tawala wa wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara
---------------------------------
Habari na picha na Abdulaziz video
Serikali ya Wilaya ya Masasi mkoa wa Mtwara, imesema kuwa uongozi
wa wilaya utahakikisha unaanza kushirikisha makundi ya watu wenye
ulemavu katika shughuli mbalimbali za maendeleo kwa asilimia 100
ikiwemo kushiriki kwenye ziara za viongozi wa kitaifa wanaokwenda
Wilayani humo jambo ambao litasaidia kuondoa dhana ya kunyanyapaliwa.
Kauli hiyo imeitolewa Jumamosi na Mhe Yahana Miwa, Katibu Tawala
wa wilaya hiyo, alipokuwa akifungua mafunzo ya mkataba wa umoja wa
mataifa (UN) kwa niaba ya mkuu wa Wilaya hiyo, Farida Mgomi.
Mafunzo
hayo ya siku tatu yanahusu sheria na sera kwa watu wenye ulemavu
mkoani Mtwara na kuandaliwa na shirikisho la vyama vya watu wenye
ulemavu (SHIVYAWATA) mkoani humo na kufanyika katika ukumbi wa mami
mjini hapa.
Mhe Miwa alisema serikali itahakikisha kwamba makundi yote ya watu wenye ulemavu
yaliyopo Masasi yanashiriki kikamilifu masuala mbalimbali ya maendeleo
ili kuyapa fursa kwa makundi hayo kuweza kutoa mchango wao katika
mambo ya maendeleo yanayofanyika Wilayani humo kama makundi mengine ya
kijamii yanavyoshirikishwa.
Alisema walemavu ni sawa na watu wasio walemavu hivyo wana haki ya
kushiriki katika masuala mbalimbali ya maendeleo yanayofanyika katika
maeneo yaliyowazunguka hivyo kuanzia serikali Wilayani Masasi inaahidi
kuanza kushirikiana na makundi ya watu wenye ulemavu bega kwa bega ili
kwa pamoja kuweza kuleta maendeleo Wilayani humo.


ni jambo la busara kwa mh YOHANA MIWAkuwashirikisha na kuwafanya wao wajione ,uwa ni sehemiu ya jamii.
ReplyDelete