Uncle michuzi asante kwa kuweka ile habari juzi ya kukamatwa mtu na madawa ya kulevya mwenye pasipoti ya Tanzania.
Sasa after the incident ya watu ambao kwa 100% tuna uhakika ni wanigeria kukamatwa na sembe na wengine kua involved kwenye cases tofauti zikiwemo human traficking and prostitution sasa wamilik wa condominiums (aina ya hosteli) mbali mbali zinazomilikiwa na Ridzuan Properties wamepitisha utaratibu huu ya kwamba hawataki tena waafrika kukaa kwenye nyumba zao.
Hivyo mzazi mwenye mpango wa kumleta mtoto wake huku au mwanafunzi mwenye mpango wa kukaa na kusoma huku especially Taylors university, Sunway university, Inti university na Segi college Subang tunawashauri ku-book hostel za chuo mapema wasitegemee kukaa nje ya hostel.
Poleni sana, Malyasia are very strict na madawa hayo. Wananyonga huko. It is clear they do not like black people, not sure people end up there.
ReplyDeleteAsante kwa taarifa mdau.Kama una muda tupe mifano hai, sisi wengine ambao hatuna idea na kinachoendelea huko, hizo "Nuisance and problems" zinazosababishwa na waafrika kwenye jamii hiyo.Lazima kuna sababu za msingi hapa.Johannesburg pale kuna jengo moja la ghorofa(la serikali?) wanaishi wanaNIgeria watupu bila kulipa,waliliteka wakaanza kuitana mmoja baada ya mwingine.Polisi hawalisogelei
ReplyDeleteDavid V
ReplyDeletelol hili tangazo nimeliona na kwenye condo yetu ya Subang Avenue nadhani sio Ridzuan peke yake bali ni Condominium nyingi sana zilizopo mitaa hii me nawaona wajinga sana hawa wachina
ReplyDeletehahahhahaha rudini nyumbani tuu msome hapa UDSM hakuna kingine huko hawa wataki kabisaaa
ReplyDeleteKAMA KAWAIDA YETU, MSHAHARIBU HUKO. SUALA HILI NI ZAIDI YA U NIGERIA NA MADAWA. WAAFRIKA UNAMPANGISHA MMOJA WANAKAA KUMI NA MOJA! ULEVI, MZIKI SAUTI YA JUU, UMALAYA NK
TUBADILIKE JAMANI
jamani haya mambo musiyachukulie kirahisi hivyo; mara nyingi kuna politics behind apart from the fact that; yes like any other people; africans are africans they have their positive and negative traits; hili suala sio tu litawagusa walioko huko hivi sasa lakini na wengine wenye plan (au wazazi wao) ya kwenda kusoma huko; na itapelekea kuongezeka pesa ambayo yoyote anaetaka kwenda kusoma Malaysia kuwa nayo; hii ni pigo kwetu; kwani Malaysia tofauti na UK na USA was still a cheaper alternative for higher education studies which have a good world reputation and recognization; wadau tuliangalie hili kwa kina na labda tufikirie vipi tutakwamuka kwenye hiki kigingi!
ReplyDeleteHivi nashindwa kuelewa inakuwaje hawa wanaigeria wanakuwa na pass za kitanzania,wanazipatajepataje?uozo huu uko wapi?mambo ya ndani?tubadilikeni jamani tuilinde nchi yetu.
ReplyDeleteMBALI NA HAYO MATUKIO YA MADAWA YA KULEVYA HAWA WATU WANA UBAGUZI SANA KWA SISI NGOZI NYEUSI
ReplyDeleteMdau wa mwisho naungana nawe.Waafrika popote walipo ni matatizo tu.Nimeishi Ulaya miaka sana nchi mbalimbali na sasa naishi hapa Asia..popote walipo waafrika lazima kuna malalamiko ya tabia chafu za ulevi,matusi,umalaya,vurugu,uchafu,uvunjaji wa sheria mfano kuvuta sigara sehemu isiyoruhusiwa,Uwajibikaji mbovu katika masomo na hata katika mambo yanayomhusu yeye mwenyewe kama usafi wa chumba chake.Na matukio mengi huambatana na uharibifu wa mali za watu kama vile kuvunja milango,kuharibu taa n.k.
ReplyDeleteHapa hakuna mambo ya mnaigeria wala m'bongo wote hovyo kabisa,nimewakuta Watanzania wengi sana nchi kadhaa wenye tabia hizi na hata wengine waliishia kufukuzwa na kurudi Tanzania.Vijana wa Kiafrika tusipobadilika na kustaarabika ipo siku nchi za watu watakataza kabisa hata kuingia tu Waafrika nchini kwao.Nyie mtabakia na haki za binadamu,."Hakuna haki bila kutimiza wajibu"..TAFAKARI NA CHUKUA HATUA
Haya matatizo ya feki Tanzanians ni lazima serikali iyaangalie na darubuni kali.Inaonyesha kuwa ni rahisi mtu kupata pasipoti ya Tanzania. Bila shaka kuna wajuzi wanaziuza maana sifikiri kama wazitoa kwa kuwaonea huruma hao wauza madawa. Wasakwe hao jamaa na pengo lizibwe.
ReplyDeleteDUUUU Na Msirudi huku Nyie waasirika Maana yaonekana Mnadhani Malaysia au Ulaya ni kwenu maana wazazi wenu wanajibana nyie mnajisahau huku, hakuna kiuwaonea huruma nyie watu wahuni hata huku tumestaarabika siku hizi SHAME on you
ReplyDeleteHasa waTZ ni uchafu mtupu....ndio maana hata hapa home tumekuwa watuongozeki, Vichwa vigumu, hakuna nidhamu......Mtoto wa kitnzania utamuona tu hata kama ni mdogo sana , cheza yake itakuonyesha kuwa ni mTZ.
ReplyDeleteSasa wakati umefika tubadirike, ingawa itachukua muda kukubalika , lakini tukijipanga vema tutawin.
Wala sio kwa sababu ya madawa ya kulevya, bali ni fujo, vurugu na matimbwili ya kila aina ndo chanzo cha kubaguliwa. Haileti maana kukamatwa kwa mtu m1 ndo iwe sababu ya kuwafanya waafrika wote wahusishwe na madawa. Kuna zaidi ya madawa hapa, ulevi, matusi, ugomvi hasa na locals, kutokua na nidham/heshima n.k ndo tatizo kubwa nnaloliona hapa. Ukiishi kwa watu basi jaribu kuishi kulingana na taratibu zao, usilazimishe taratibu za nyumabni kwako ukiwa nyumbani kwa watu.
ReplyDeleteSitetei hali hii na nakemea vikali kabisa lakini hata wale wazungu waliomwagiwa tindikali Znz wangeshimu tamaduni za wazenji hasa ktk kipindi cha mfungo huenda wasingemwagiwa tindikali!!
Nmeishi Asia na nlijitahidi kufata tamaduni nao nlionekana tofauti na waafrika wengine kitabia na landlord wangu alinikubali sana. So tukibadilika na kufata taratibu za wazawa ni hakika hatutagombana na mtu duniani. Ubaguz upo but sometime ni wa kujitakia wenyewe!!
1-''MASOGANGE'...a.k.a Madawa ya Kulevya.
ReplyDelete2-''JOG JIG''...a.k.a Uzinzi na Umalaya
3-''UKWAPUZI''...a.k.a Wizi.
Ustaarabu hauna shule !
Licha ya kuwa makosa yanafanywa na Waafrika wenzetu Wanigeria wakitumia Pasipoti za Tanzania na kusomeka kama Watanzania , all is all Waafrika tuna hulka mbaya sana ya mambo hayo matatu hapo juu, ingawa HULKA hizi zinafanywa na races nyingine (watu wa rangi zingine) wenzetu mambo haya ya Fedheha angalau wanafanya kwa kujificha sana. LAKINI SISI TUNAFANYA BILA YA WOGA WALA AIBU.
MATOKEO YAKE SASA WOOOTE TUNAONEKANA TUMEKUNYA!!!
MNAWABAGUA KWA UNIGERIA WAO NANYI MNABAGULIWA KWA UAFRIKA WENU, NGOMA DROO!
ReplyDeleteNakubaliana na wale walioelekeza haja ya sisi wenyewe kubadilika. Waafrika tuko kama limpukeni limpukeni hivi. Mtu akienda nje anaona tena yeye tu, anaishia kufanya mambo ya kijingajinga tu. wenzetu duniani wanatafuta maisha , sisi uhuni tu na kutaka njia ya mkato ya kuwahi maisha. Ukipanda mtama utavuna mtama na sio vyenginevyo. Dawa iliyobakia mrudi nyumbani tu, tuje kugawana huo ujinga. Kama hatukugeuka tutabakia vibarua haadi mwisho wa dunia.
ReplyDeleteNakubaliana na wote wanaosikitishwa na tabia zetu huko ugenini. Tabia zetu ni mbaya hata nyumbani. Sema tu kwa kwa vile nyumbani ndio tunavyoishi, basi kila mtu anaona ni kawaida tu. Na mimi nimekaa Ulaya, Amerika na Asia. Waafrika wana vurugu sana. Utakuta mtu anafungulia muziki kama yuko kisiwani mwenyewe. Hafikirii majirani zake. Ukiwambia anajibu kwa ngumi. Nyumba za watu tunachafua. Nyumab za watu tunazifanya mageto na kujazana kwenye kichumba kidogo. Halafu tungi juu na ngono. Choo kama ni cha kuchangia, Waafrika wengi huacha kikiwa kichafu baada ya kutumia. Waasia kwa asili yao ni watu wastaarabu sana. Hawapendi vurugu. Hapo watakuwa wamechoka kabisa na wanaona hakuna njia nyingine. Tatizo ni jinsi tunavyolea watoto wetu. Sehemu ambayo Waafrika wanaweza kuishi bila mgogoro mkubwa ni USA kwa vile kuna Afro-Americans ambao pia tabia hizo chafu zimewashinda kuacha hata baada ya kukaa huko kwa vizazi na vizazi.
ReplyDeletemalaysia sio watu wazuri kabisa..mimi nimesoma huko miaka mitano na namshkuru Mungu nimemaliza salama..huko ubaguzi ni wa hali ya juu..hakuna lolote la maana...wanafikia mpaka kukuua jus bcoz ur black..Never Go To Malaysia
ReplyDeleteSs ni ule wakat ambao wazaz woteee waone umuhimu wa kuboresha elimu ya bongo ili wsipeleke watoto nje,,na hao wengine wa nje waweze kuona umuhimu wa kuleta watoto huku...mzaz unampeleka mtoto shule anasoma huko miaka6,,hujawah hata kwnda kuona anaishje,mazingra gani ana rafk wa aina gani,,ww unajua tu kutuma ada na nauli za likizo na matumiz.,mtoto kuingia chuo sio kumaanisha kakua na ahitaji uangalizi wa mzaz,,labda had aoe au aolewe wataangaliana na spouse wake..kuna wengne had anashika mimba anazaa huko akija bongo unaona tu mtoto kanenepa unasema kumempenda kumbe analea nch za watu...
ReplyDeleteIfike mahali tuanze kupenda vya kwetu..kama tunaona vyuo vyetu havina hadh bas na tuviboreshe.tatzo kubwa ni wanaoenda huko weng hawana viwango vya kusoma vyuo vyetu vya bongo.