Mkutano wa Kumi (10) wa Baraza la Mawaziri wa Sekta ya Miundombinu, Mawasiliano na Hali ya Hewa unatarajiwa kufanyIka tarehe 23 Agosti, 2013 jijini Kigali. Mkutano huo umetanguliwa na Mkutano wa Wataalamu kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kuanzia tarehe 19-21 Agosti 2013 ambao utafuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu utaofanyika tarehe 22 Agosti, 2013.

Baraza la Mawaziri wa Sekta ya Miundombinu, Mawasiliano na Hali ya Hewa linategemea kupokea taarifa ya utekelezaji wa Programu na Miradi mbali mbali inayotekelezwa katika nchi Wanachama katika Sekta za Barabara, Reli, Bandari, Hali ya Hewa, Mawasiliano, viwanja wa ndege pamoja na utekelezaji wa maagizo ya Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama ya waliyoyatoa katika Retreat yao ya pili kuhusu ufadhili na maendeleao ya Miundombinu pamoja na maagizo ya Mkutano wa tisa ( 9) cha Baraza la Mawaziri wa Sekta husika wa tarehe 24 Februari, 2012.

 Baada ya kupokea taarifa husika Baraza la mwaziri linategemea kutoa miongozo na maamuzi ya kisera.
Mkurugenzi wa Miundo Mbinu katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Ndugu Wambugu 
(kushoto) akiwasilisha taarifa ya utekelezaji, anayefuata ni Naibu Katibu Mkuu anayehusika na Mindombinu Ndugu Enos Bukuku.
Maafisa Waandamizi kutoa nchi Wanachama wakifuatilia kwa makini Mkutano husika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Tanzania yajitoa ushirikiano wa Afrika Mashariki! picture speaks volumes!

    ReplyDelete
  2. hahahahahahaha labda alitoka kidogo kuchimba dawa.

    ReplyDelete
  3. Mara zingine bora tujitoe!


    Hata katika maisha ya kibinaadamu ya kawaida huwezi kufika mbali kama utashirikiana na mwenza Mnafiki na mwenye Agenda ya Siri na hujuma dhidi yako.

    Nchi kama Kenya na Rwanda wao wanawaza zaidi kunifaika kutoka Tanzania kuliko Tanzania kunufaika kutoka kwao.

    Sasa huo ni ushiriakiano wa namna gani?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...