Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kumpongeza Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax, kwa kuteuliwa na Viongozi Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kuwa Katibu Mtendaji wa Jumuiya hiyo katika Mkutano wa Viongozi Wakuu hao tarehe 18 Agosti, 2013, Jijini Lilongwe, Malawi.
Uteuzi wa Mhe. Dkt. Tax katika wadhifa huo mkubwa na nyeti sio tu ni fahari kwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ambako amekuwa Katibu Mkuu, bali pia kwa Watanzania wote. Tanzania kama mmoja wa nchi waanzilishi wa SADC na mshirika muhimu, inajisikia fahari kwa kushika nafasi hii ya Katibu Mtendaji. Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax anaondoka akiwa na mafanikio makubwa katika Uendelezaji wa Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki inamtakia, Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax, kila la kheri katika majukumu yake mapya na inajivuna kwamba SADC imepata Kiongozi shupavu, mahiri na mchapa kazi.
Imetolewa na
WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
Nilidhani Morgan Tsvangirai
ReplyDeleteDavid V