Na Elvan Limwagu wa Globu ya Jamii,Masasi 

Basi dogo la kubeba abiria liitwalo BUTI LA ZUNGU lenye Namba za Usajili T510CFM aina ya Toyota Costa jana (18/8/2013) lilikamatwa na Polisi maeneo ya Njenga Ndanda na kufikishwa katika Kituo cha Polisi Ndanda baada ya kupekuliwa na kukutwa na Madumu 5 ya Pombe haramu aina ya Gongo yakiwa yamefichwa chini ya siti.

Madumu hayo ambayo yalifungwa vizuri ndani ya mabox na juu yake kufunikwa kwa mifuko myeusi ya nylon pasipo kutoa harufu kabisa.

Basi hilo linalofanya safari zake kati ya Lindi – Masasi lilikamatwa majira ya saa 9 alasiri likisafiri kutoka Masasi kwenda Lindi. Baada ya upekuzi mmiliki wa mzigo huo hakujitokeza na Makondakta walishindwa kumtaja mwenye mzigo huo na hivyo Kondakta mmoja aitwaye ALLY alishikiliwa katika kituo hicho kwa kuisaidia Polisi. Basi hilo ambalo lilibeba abiria nikiwemo “mimi” liliruhusiwa kuendelea na safari saa 9:55 alasiri.
Askari Polisi wa Kituo cha Ndanda wakiendelea na ukaguzi kwenye basi hilo.
Mara madumu kadhaa yakaonekana na kuanza kushushwa.
Hili ndio basi lenyewe lililokuwa limebeba kilaji hicho haramu.
Hivi ndivyo kilivyokuwa kimehifadhiwa kilaji hicho,tena kwa ustaji mkubwa ili kisibainike.
Wadau wakidiskasi jambo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Supu ya Mawe lita 5!

    Ohhh Kusini huko Masasi Mtwara na Lindi hayo si Majanga majanga, kwa supu gani ya nyama inayo patikana Mikoa ya Kusini kwa ukosefu wa mifugo kama ng'ombe na mbuzi kuweza kupoza Makali ya Gongo a.k.a Konyagi B?

    Huko si ndio kuunguziana Mapafu na kupunguziana urefu wa maisha wakati Lindi yenyewe Vitoweo ni Samaki wakavu ama wa mchuzi chuku chuku wakiwa hata mafuta hawana?

    ReplyDelete
  2. Gongo ni kinywaji cha kawaida kabisa ktk vijiji vyetu na kila mmoja anakunywa, wakulima wachache sana wanaoweza kupata shs 2,000 kununua bia moja. Huo ndio ukweli na askari wanajua hilo!

    ReplyDelete
  3. aaa kwa jinsi ilivyokuwa packed kwa ustadi si bure kuna watu wa karibu wamechoma dili.

    ReplyDelete
  4. Gongo ni kinywaji ambacho wananchi vijijini wanaweza kumudu. Nashauri serikali iruhusu watengenezaji na kiwekwe kitengo cha kuthibiti ubora wake.Hii ni kutokana kwamba baadhi ya watanzania walisoma shule kutokana na wazazi baadhi ya wazazi wetu kufanya biashara ya gongo hasa wakina mama.

    ReplyDelete
  5. Mdau wa 4 suala hili linahitaji kufikishwa kwa Ndugu Mgwasa Mkuregenzi Mtendaji wa KONYAGI-A Kampuni ya TDL.

    Labda anaweza kupigania hawa wenzeke wa Msituni wapewe Leseni halali ya uzalishaji kama yeye!

    ReplyDelete
  6. Ohooo nini tena?

    Masihara hayo Mamwinyi wa Kusini Lindi na Mtwara, ni wiki moja tu iliyopita mmetokea ndani ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu kipindi ambacho hakuna mwana Kusini hata mmoja ungemshirikisha ktk Mpango huo akakubali!

    1.Kama ni Abiria hakuna ambaye angekubali kupanda gari hilo ktk Mfungo!

    2.Kama ni Kondakta asingekubali kupiga mzigo kubeba bidhaa hizo huku akiwa na Swaumu hata Shanta ama Dei waka wa Basi ansingekubali!

    3.Kama ni dereva asingekubali, endapo Bosi wa basi angempa kazi hiyo dereva angekuwa tayari kuchomoa Kibandiko chake (KOFIA YA BARGASHIA) mfuko wa nyuma wa suruali yake za akakichomeka ktk Kisogo cha kichwa chake na akakabidhi funguo za Basi LA BUTI LA ZUNGU kwa Bosi huku akinyanyua mikono juu akiomba kwa Mwenyezi amjaalie apate kazi nyingine!

    Sasa leo hata wiki ya pili haijaingia toka Mfungo uishe huku (THAWABU MLIZO CHUMA NDANI YA MFUNGO HUENDA HAZIJA WASILI KWA MWENYEZI) mmesharudi kwenye Mipango ya Magongo tena?

    ReplyDelete
  7. Hehehehe !!!

    Hii kubwa!

    Jina la Basi lenyewe (BUTI LA ZUNGU) na mzigo lililobeba (GONGO) sawasawa!

    Maana tayari wana Kusini mna jina mbadala la Gongo mkiita NIPA kitu ambacho ahata Polisi atakayehamia kutoka Mkoa mwingine wa mbali akija Mtwara na Lindi mtakuwa mmemuacha kwa jina hilo atakuwa hajui ni nini!

    Au wana Kusini Buti la Zungu ndio jina Jipya la Gongo?

    ReplyDelete
  8. Endapo ulevi ungekuwa unakipmwa kama UMEME, basi nadhani hili Gongo lingekuwa kwa uzito limepitiliza vipimo!

    Mfano

    1.Maji ya kawaida ya kunywa yatakuwa na VOLTAGE 0 kwa ukali!

    2.Bia na Pombe zingine za kawaida zingekuwa na VOLTAGE kama 100 hadi 500 , au 600 hivi!

    3.Lakini hili GONGO nadhani litakuwa linasomwa ktk Vipimo kama KvA AU MEGAWATI kuanzia 100,000 kwenda juu!!!

    Lile Gongo lilololeta maafa la Kigogo Mbuyuni Dar nadhani lingefikia MEGAWATI BILIONI MOJA AU ZAIDI!...Tanesco ingepata chanzo mbadala cha umeme Kigogo!

    Gongo inaeleweka ni zaidi ya Konyagi!!!, karatasi ikiloweshwa gongo ikiwashwa inaungua, maini ya Mnywaji yanaungua kama karatasi!

    Gongo mchezo?

    ReplyDelete
  9. David Mgwasa!,

    David Mgwasa!,

    David Mgwasa!,

    Mkurugenzi wa Konyagi!


    Wezi !

    Wezi!

    Wezi!

    Wezi wa kazi zako Mikoa ya Kusini haooo, Lindi na Mtwara!

    Angalia Wezi wa haki miliki haooo!

    Mkurugenzi wa Konyagi umeona hiyo?

    Angalia wameiba hadi Formula ya bidhaa zako wameingia miferejini na vichakani wamezalisha mzigo na sasa wanakwenda uuza mijini!

    Angalia unafanyiwa Usanii na kuibiwa Haki Miliki ya Nembo yako!!!

    Angalia wanatumia Makasha na Maboksi ya Konyagi kusafirishia Gongo lao!!!

    ReplyDelete
  10. Kwa Pombe za namna hii ndio maana maisha yanakjuwa mafupi Tanzania na watu wanazeeka kwa kasi ya ajabu kabisa!

    Unakutana na Kijana wa Miaka 19 akiwa anakunywa mambo haya anakuwa kama ana umri wa Miaka 91!

    ReplyDelete
  11. Jee unajua kuwa GONGO ilikuwa hairuhisiwi nchini na wakoloni kwa sababu walikuwa wanaprotect biashara zao za whisky Johny Walker na brandy zao. Sasa mkoloni kisha ondoka tupe sababu nyingine za kuwakataza wananchi "kula" gongo

    ReplyDelete
  12. Tulizoea kusikia habari za gas Mtewara,hii ya Gongo tena mlotuletea leo ni mpya kabisa!

    ReplyDelete
  13. Hahahahaha

    Mdau wa 6 hapo juu: Ohooo nini tena?


    Hapo Dereva wa Basi Buti la Zungu angekabidhi Funguo kwa mmiliki wabasi akasela ASSALAMA LEKO SHEHE siwezi kubeba Gongo lwenye gari nimefunga Mwezi Mtukufu aku siwezi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...