Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akimkabidhi Bendera ya Taifa,Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred (katikati) anaetarajiwa kuondoka hivi karibuni kwenda nchini Indonesia kushiriki Mashindano ya Urembo wa Dunia (Miss World 2013).Kushoto ni Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania,Mh. Emmanuel Ole Naiko.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania,Hashim Lundenga akimuaga Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred (katikati) mara baada ya kukabidhiwa Bendera ya Taifa na Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara  (kulia) wakati wa hafla ya Chakula cha jioni kwa ajili ya kumuaga Mrembo huyo,iliyofanyika kwenye Hoteli ya Giraffe,Jijini Dar es Salaam usiku huu.
 Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara (wa pili kulia) akitoa nasaha zake kwa Warembo wanaowania taji la Redd's Miss Tanzania 2013,wakati wa hafla ya Chakula cha jioni ikiwa ni sehemu ya kumuaga Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred (pili kushoto) anaetarajiwa kuondoka hivi karibuni kwenda nchini Indonesia kushiriki Mashindano ya Urembo wa Dunia (Miss World).Hafla hiyo imefanyika usiku huu kwenye Hoteli ya Giraffe,Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Herman Mwasoko na kushoto ni Mlezi na shoto ni Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania,Mh. Emmanuel Ole Naiko.
Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred akikumbatiana na Mama yake Mzazi wakati wa Kumuaga.
Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred akitoa shukrani zake wakati wa hafla hiyo ya kumuaga iliyofanyika usiku huu kwenye Hoteli ya Giraffe,jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Warembo wanaowania Taji la Redd's Miss Tanzania 2013 wakiwa kwenye hafla hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mmmmmh god's glory! Hata mama yake naye nastahiki kuingia kwenye hiyo beauty contest na kuwa miss jamani.

    ReplyDelete
  2. Verdiana Mashingia mama mtoto kashine kweli kweli kama binti. Hongera mama kwa kuzaa chema.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...