Hii ndio safari ya Mwisho ya Dada yetu Nemela Phillip Mangula aliezikwa jana huko Kijijini kwao,Mkoani Njombe na mazishi yake kuhudhuliwa na watu mbali mbali.
Baba mzazi wa Marehemu Nemela,Mzee Phillip Mangula akisoma wasifu wa Marehemu mwanae wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika jana huko kijijini kwao,Kushoto ni Mama Mzazi wa Marehemu.
Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM ambaye pia ni Waziri wa Nchi ofisi ya Rais mahusiano Uratibu wa sera Mhe. Stephen Wasira akitoa salamu za Chama wakati wa Mazishi hayo.
Baadhi ya viongozi wa Chama,Serikali na Bunge walishiriki mazishi ya Nemela Phillip Mangula huko Mkoani Njombe.
Viongozi wa Chama kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Vijana Taifa Mhe. Sadifa , Mwenyekiti wa Wazazi Taifa Ndg. Bulembo, Mjumbe wa NEC -Temeke Ndg. Magesa na Katibu wa uchumi wa Vijana wakijadiliana mambo muhimu ya Kitaifa huko Mkoani Njombe wakati wa mazishi ya Nemela Phillip Mangula.
Mwenyezi Mungu akujalie pumziko la milele Nemela gone too soon!Daima utakumbukwa na wana CFR- MFR wenzio.
ReplyDeleteKwa wazazi inauma sana,yaani sana kumlea na kumkuza mtoto miaka yote hiyo and then anakutoka ghafla katika umri kama huu.Pole sana Mzee Mangula na wewe mama yake mzazi kwa ujumla.Pole na wafiwa wengine, ndugu jamaa na Marafiki.
ReplyDeleteDavid V