FAMILIA ya Mzee Augustino Mgonja wa Pugu Kajiungeni Dar es Salaam na Familia ya Marehemu Bwana na Bibi Henry Kitosi (Mwakitosi) wa Iringa zinasikitika kutangaza kifo cha Mtoto wao, VICTORIA KITOSI  (DOTTO) kilichotokea Alfajiri ya leo Agosti 22, 2013 katika Hopitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam alikolazwa baada ya kuugua ghafla.

Mipango ya Mazishi inafanyika Pugu Kajiungeni nyumbani kwa Mjomba wake Agustino Mgonja.

Habari ziwafikie, Mama Mdogo wa Marehemu, Mary Nathan wa Kinyenze Kipera Mkoani Morogoro, Kaka wa Marehemu Bosco Kitosi wa Mwanza,Doris KitosiA wa Iringa, Bibi wa Marehemu,Balozi  Christina Shogholo wa Kisiwani Same-Kilimanjaro, Mjomba John Mgonja wa Kabuku Tanga, Ukoo wote wa Mwakitosi na Shogholo, Ndugu Jamaa na Marafiki popote pale walipo.

Marehemu ameacha Mume na watoto wawili, Sanden na Sabri.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE. AMEN.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Poleni sana wanafamilia na ndugu wote na marafiki na jamaa katika kipindi hiki kigumu.

    Nimesikitika sana kupata habari hizi, na machozi yamenindondoka kwa uchungu sana.

    ninamfahamu Vicky, walikua jirani zangu Iringa pale Mkimbizi.

    Raha ya milele uumpe ee bwana na mwanga wa milele umuangazie, apumzike kwa amani.

    ReplyDelete
  2. BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE

    ReplyDelete
  3. Pumzika kwa amani Vicky tulikupenda ila Mungu amekupenda zaidi.

    ReplyDelete
  4. R.I.P Vicky

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...