TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Taswira ya Zanzibar kama kisiwa cha amani imechafuliwa tena jana usiku pale watu wasiojulikana walipofanya kitendo cha kinyama na kishenzi cha kuwamwagia tindikali (acid) wananchi wawili wa Uingereza katika maeneo ya Shangani, jimbo la Mji Mkongwe.
Taarifa za awali nilizozipata ni kwamba vijana hao wawili wapo Zanzibar wakiwa ni sehemu ya vijana wanaojitolea (volunteers) katika shughuli za sanaa (Arts).
Nikiwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe, mwananchi wa Zanzibar ninayeipenda nchi yangu na pia nikiwa kama binadamu ninayethamini utu wa kila mtu nalaani vikali na kwa nguvu zote uovu na uhalifu huo ambao umekiuka misingi ya ubinadamu na utu.
Polisi na mamlaka nyengine za nchi zinapaswa kufanya uchunguzi wa kina na wa haraka wa kuwajua ni nani waliohusika na tukio hili na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria. Hili la kuchukua hatua za haraka na za dharura na kuongeza kasi ya uchunguzi ni la muhimu sana maana sasa matukio ya hujuma kwa kutumia tindikali (acid) yamekuwa ni jambo la kawaida na yanaendelea kuongezeka.
Tukio hili la jana linakwenda moja kwa moja na kupiga moyo wa uchumi wa Zanzibar kwa maana ya sekta ya utalii. Tusipochukua hatua za haraka na za dharura na kuonekana tunajali, uchumi wa Zanzibar unaweza kuathirika kwa kiasi kikubwa na kuyumbisha utoaji wa huduma kwa wananchi, huduma ambazo zinategemea mapato yanayotokana na utalii.
Nilipata nafasi ya kufika haraka pale walipokuwepo waathirika wa tukio hilo mara baada ya kupata taarifa na pia kuwasindikiza hadi Uwanja wa Ndege wa Zanzibar nikiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na

Michezo, viongozi wa Jumuiya ya Wawekezaji katika Sekta ya Utalii (ZATI) na Balozi wa Heshima wa Uingereza aliyepo Zanzibar. Nawapa pole wasichana hao wawili na nawaombea wapone kwa haraka. Fikra, hisia na dua zetu ziko pamoja nao. Sifa ya Zanzibar kwa karne nyingi imekuwa ni kisiwa cha amani ambacho watu wake ni wastaarabu, wakarimu na wanaopenda wageni. Mjengeko wa jamii ya yetu ya Kizanzibari wenyewe umetokana na mchanganyiko wa watu kutoka sehemu mbali mbali duniani ambao walihamia Zanzibar na kupafanya ndiyo maskani yao. Kitendo kama hichi kilichotokea jana kinakwenda kinyume na misingi ya historia yetu hiyo.
Ni mapema kusema ni nani aliyepo nyuma ya kitendo hichi lakini jambo moja la wazi ni kuwa yeyote anayehusika amekusudia kuiumiza Zanzibar na Wazanzibari. Kuuhujumu utalii ni kuuhujumu uchumi wa Zanzibar na kuyahujumu maisha ya Wazanzibari. Wakati mamlaka zinazohusika zikiendelea na uchunguzi wa tukio hili, kuwasaka waliohusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria, natoa wito kwa Serikali kuchukua hatua zifuatazo:
Mwisho, natoa wito kwa wananchi na wakaazi wote wa Mji Mkongwe na Zanzibar kwa ujumla kuwa makini na kufuatilia nyenendo zinazotia mashaka au zinazoashiria mwelekeo wa kufanya vitendo vya uhalifu ndani ya Mji wetu na ndani ya Zanzibar au hata nje ya Zanzibar na pale wanapobaini mwelekeo kama huo kutoa taarifa haraka kwa mamlaka zinazohusika. ISMAIL JUSSA MJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI JIMBO LA MJI MKONGWE a na Jumuiya ya Wawekezaji katika Sekta ya Utalii (ZATI) na Jumuiya ya Watoa Huduma za Usafirishaji na Utembezaji Watalii (ZATO) ili kushughulikia matatizo mbali mbali yanayojitokeza hususan yale yanayohusu masuala ya usalama wa wageni wanaotembelea Zanzibar.

Maradhi ya roho ni mabaya kuliko hata maradhi mengine tuliyoyazoea.Wafanyao vitendo hivi popote pale, iwe nchini Zanzibar(Mji mkuu ni Mji Mkongwe)au hata nchi ya Tanganyika(Dodoma)ni wagonjwa wa maradhi ya roho,Maradhi ambayo hayatambui wala kuona utu wa binadamu mwengine.
ReplyDeleteZanzibar bado ni ya wastaarabu lakini kuna mijitu imejaa chuki na wala sio watu wa bara ni wa unguja na wapemba wenyewe kila baya wao hupenda kusingizia muungano na watu wa bara sasa wana kulana wenyewe kwa wenyewe.
ReplyDeletewalianza na mashehe na wakafuatia kuuwa padre wa kichaga wakaona bado wakamwagia tindi kali sheha wa ccm wa tomondo.
sasa wameona bora watalii wazungu tena wasichana.
wakitoka hapo watawamwagia mawaziri wao ccm na cuf hiyo ndio hali halisi ya Zanzibar.
na tafadhalini msisingizie bara huu ni uchafu wenu wenyewe kama dini ndio inayowatuma semeni wazi kama siasa ndio inawatuma semeni wazi lakini msiseme uwongo wa kuwasingizia watanganyika sisi hatuna haja na nyie vile vile hivyo msifikirie sote tuna taka muungano semeni ni hao ccm wenzenu sisi chadema tumeshasema wazi kila mtu kwao.
mpemba yoyote mwenye duka nyumba hapa dar awe tayari kulipa ushuru kabambe wanaolipa wataliana hapa kwani wote wageni.
kazi kwenu mdebwedo.
mdau.
dares salaam.
Kwani nyie wabara hamujui kama wapemba ndiyo wanawaweka mjini
DeleteHaya kufanyika wakati wa Iddi si kutushambulia sisi sote kama Taifa lakini kudhalilisha imani zetu sote za kuheshimu na kusherehekea dini zetu zote
ReplyDeleteNasiitiza tena it is no longer peaceful in both Tanzania mainland na Zbar. We should stop this hypocrisy jamani. Watanzania wengi ni wanafiki, waongo, wezi na wajinga. Roho za chuki, wivu na ukatili zimetwala. Period
ReplyDeleteVyombo vya usalama, Polisi na wakazi , mji wa zanzibar ni mdogo na watu wanajuana kuna uwezekano mkubwa wa kuwakamata wamwaga acid tatizo kazi ya ukachero inabidi ifanywe kwa kiufundi, busara na kwa jitihada zote kurudisha jina la zanzibar vile vile patrol na camera ni muhimu sana kama alivyosema mwakilishi
ReplyDeleteJamani mnasema Zanzibar tu kwa kuwa waliomwagiwa ni wazungu mbona wengi wamemwagiwa huku Tz bara mana wote ni binadamu! utu hakuna tena kwa sasa iwe Zanzibar iwe bara hakuna utu. Jana nimesoma mhadhiri wa UDSM ameuawa kwa risasi mchana magomeni sasa hii ni nini? Mana hizo hatua za polisi hata wachukue watu waishakufa na wengine wa tindikali kudhurika vibaya, hivi vyote vinatakiwa visitokee kuwe na prevention measures toka kwenye vyombo vya usalama iwe polisi na vinginevyo. Yani kwa sasa Tz. watu wanaishi kwa uoga kwamba chochote kinaweza kutokea wakati wowote si unapokuwa njiani, kwa miguu au unaendesha gari watu wanabuni njia mbaya sana za kuuawana kutumia pikipiki nk. Sijui polisi waongezwe watu wapewe mafunzo ili ulinzi uimarishwe kila kona ya nchi, na hao polisi walipwe vizuri ili wasiwe na tamaa ya hongo. Tanzania bila uhalifu inawezekana, ni wakubwa kuamua tu mikakati ipi itumike. Mkishindwa tafuteni misaada nje kwa kuuliza jinsi gani wenzetu wanaimarisha ulinzi katika nchi zao. Kuhusu acid nilisoma watu wanalalamika wanaouza, jamani muelewe kuwa acid ina source nyingi hata maji ya betri za magari ni acid, hapo mnazuiaje kuuza acid? pia watu wanaweza kutengeneza wenyewe. Iko trick sana ni watu kuacha uhalifu na sio kuuza au kununua, ukiwa na betri iliyokufa ina maji ya acid hapo utasemaje? Au tuanze kutumia betri za magari zisizo na acid kabisa na how about mabetri ya tochi, taa za betri nk, hivi hapo unazuiaje hilo soko. Mungu tu aingilie kati aiponye tz.
ReplyDeleteIlisha hamasishwa, Usipolipiza kisasi kwa makafiri kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani, utalipiza lini?
ReplyDeleteLeo Mnawasaka watekelezaji badala ya wahamasishaji.
Hata mkibaki wenyewe tupu mtaendelea kuuana hivyo hivyo. Tazameni nchi za wenzenu.
Mdau
Tulivyo wazembe patrol iztzpamba moto kwa muda tu kisha kahawa kama kawaida, kamera zitaisha betri na kukaa kama pambo tu. Patrol na kamera ziwe akili zetu. Unadhani waliofanya kitendo hicho hawakuonekana na watu? Hii nchi ni yetu tuipende si kwa mdomo tu. wengine hatuna mjomba nje tukimbilie huko.
ReplyDeleteMungu ilinde Amani yetu, warudishie imani ya Utu wa iliyowapotea. Semeni hadharani matatizo yatatuliwe kwa Amani. Enyi waja wa Mola muwe na subira, ya nini kuwadhuru wengine kwa sababu wasizozijua.
ReplyDeleteMungu ibariki Tanzania
KWELI KABISA NAAMINI KWA UPANDE WA UCHUMI LAZIMA,INAWEZEKA UKAPUNGUA KWA %% FULANI,MAANA KUMETENGEZWA SURA MBAYA KWA WALE AMBAO WANATAKA KWENDA ZANZIBAR ILI WAKATALII
ReplyDelete®:©©
Nilisikiliza mahojianao na kwamba huenda sababu ni kuvaa vile dini ya kiislamu isivyotaka. Ikiwa sababu ni hiyo,nasisistiza, ikiwa hiyo ndiyo sababu ya kumwagiwa tindikali,Nadhani ni vizuri ifike mahali watanzania isiwe tu tunadai haki wakati hatuheshimu haki za watu wengine. Ni vibaya sana kwenye hii dunia ya utandawazi kutaka watu wafanye vile unavyotaka wewe,ndi maana sisi wapigania haki za binadamu tunasema tuwe na religious tolerance(kuvumiliana katika dini) na hata mambo mengine kama siasa. Kumtaka mtu avae vile unavyotaka wakati siyo code of dressing kwa imani yake it is unreasoanable and unacceptable.Ni kwa misingi hii hii Papa alisema majuzi kwamba ingawa kanisa katoliki halikubali ushoga lakini ni makosa kuwaua watu ama kuwabagua kwa kuwa ni mashoga.Kinachotakiwa ni kuishi kwa mfani ili hao watu wavutiwe na kumrudia Mwenyezi Mungu.Kwa mfani itakuwaje ikiwa wakristo watataka kila mtu avae rozari?Ni vizuri sana kufanya yale dini zetu zinatutka ikiwemo kuonyesha kwamba tuna msimamo gani lakini si kuwataka watu ambao imani zao haziwaamuru wafanye hayo mnayotaka.Zanzibar inapokea watalii na pia hao wafanyakazi kutoka mataifa mbali mbali,unategemea kweli wavae vile wanavyotaka ili kufuata dini yako in this globalized world? You need to accomodate others religious belief and religious tolerance.Mtu hataenda peponi kwa kuwaadhibu watu waliovaa isivyotaka dini yake bali kwa matendo yake.
ReplyDelete