Wasichana rais wa Uingereza Katie Gee and Kirstie Trup wakipelekwa Dar es salaam baada ya kumwagiwa tindikali huko Zanzibar juzi. Hivi sasa wako njiani kuelekea London, Uingereza, kwa matibabu zaidi na kurejea kwao baada ya kufanya kazi za kujitolea kama waalimu huko Kisiwani. Shambulio hili linatangazwa na vyombo vyote vikubwa duniani na tayari vimetia doa pamoja na alama ya kujiuliza kwa visiwa vya Zanzibar
Home
Unlabelled
wasichana raia wa Uingereza waliomwagiwa tindikali wakipelekwa Dar es salaam kwa matibabu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




Serikali inatakiwa kuelimisha jamii kuhusu thamani ya watalii na watu wanao jitolea kuja kufanya kazi bila malipo yyte. Inasikitisha na kushangaza kwa yaliyotokea..huu sio utamaduni wa mtanzania kufanya hivi..sijui tunako enda ni wapi.mungu saidia tz.
ReplyDeleteWhere are we heading......?
ReplyDeleteDavid V
Mbaya sana
ReplyDeleteHii Ni balaa kubwa.
ReplyDeleteHata hivyo mimi naamini kuwa ukweli utatoka hadharani hapo mbele. Kwanza hawa vijana vamekuwa Zbar chini ya wiki mbili, na katika wakati huo nasikia kuwa wameisha kuwa na matatizo na wananchi mara tatu hivi.Kisha nasikia walikuwa wanaimba, walikuwa wanaimba nini na saa ngapi, na hao waliowapeleka Zbar jee, waliwaambia kuwa ni wakati wa mwezi mtukufu wa ramadhani? Watu wapenda kutupa jina baya, na tukio hili limeripotiwa round the world, but the truth will come out one day.
serikalu ielimishe nini? ?kwani nani asiyejua hakuna ninadamu anayetakiwa kumwagiwa tindikali? way foward serikali inatakiwa kusaidia kukamatwa kwa waliohusika.
ReplyDeleteelimu ahera bila elimu dunia
ReplyDeleteJe wale wanouwa Albino vp ? mapadri wamo na wao elimu gani ? dunia au akhera au zote ? wacha kila kitu kukipeleka kwenye udini wewe...je huko Zanzibar hakuishi wakristo ? au ndo kama muuwaji wa Norway , mwanzo walisema gaidi kwa kudhania alikuwa muislamu , walipoona ni mkristo wa mrengo mkali wakasema ana matatizo ya akili na sio gaidi na sio kitendo cha ugaidi....waliofanya wawe waislamu au wakristo ni washenzi tu !
DeleteTanzania hakuna amani tena, tindikiali sio tu kwa wageni na kwa wenyeji pia na watu kuuawawa mara kwa mara. Yani ndani ya nchi hakuna amani kabisa, tuanze kutafuta ukimbizi sasa. Sijui serikali inaenda wapi. Majanga ukichangaya na madawa ya kulevya mh Tz inatisha kwa sasa. Mungu aiponye Tz.
ReplyDeleteHayakuanza keo haya ila kwa upuuzi wa wasimamizi hali hii inaendelea. Nikikumbuka kauli za polisi siku alipouawa padre nakosa imani na utawala wa sheria huko. Hakuna aliye salama.
ReplyDeleteSerikali iamuru sheria mpya iwekwe ya adhabu kali zaidi sana kwa yeyote atae tumia tindilali kumwagia mwenzie. Pia viongozi wadini waziidi kuelimisha jamii maswala ya jazba au hasira nini na athari zake, na kwa ujumla athari baada ya tukio km hili. Unamtia machungu na kilema cha kudumu binaadamu mwenzio wewe kama nani?
ReplyDeleteHiki kikundi cha wahalifu hawa wa acid kipo zanzibar na kinafahamika na baadhi ya watu zbar. Aidha baba au kaka au mama au dada wanajua ni kaka yao, mume, mjomba au mtoto wa ndio wanafanya uhalifu huu mbaya sana. Idara ya usalama wa taifa ni dhaifu sana na upelelezi ni dhaifu sana ndio maana ni muda sasa hakuna mafanikio ya kuwakamata au kuzuia matukio kama haya. Zbar ni ndogo sana, wakiamua kumtafuta nzi utampata tu lakini udhaifu ndio unazuia. alexbura dar
ReplyDeleteWewe unayesema Watu wasiiimbe unaakili finyo sana!!! Cha maana ni Watu kuheshimu utu. Mtu aimbe asiimbe hatakiwi kumwagiwa tindikali wala soda wala maji!!! Huo ni UGAIDI. Na hii itaharibia Tanzania jina kabisaaaa. Tunaelekea pabaya sana.
ReplyDeleteNdugu yangu hapo juu nakunukuu "Watu wapenda kutupa jina baya, na tukio hili limeripotiwa round the world, but the truth will come out one day."
ReplyDeleteNdugu yangu nakuhisi unajaribu ku-justify "uhalali" wa kufanya tukio baya la acid-attack kwa hawa watalii. Ngoja nikwambie wazi, hakuna katika dunia hii ya leo justification yoyote ya mtu au kikundi cha watu kummwagia acid mtu au watu, awe mtalii au si mtalii kwa vile ametofautiana kiitikadi za kisiasa, kidini ama kimaadili. Haya ni matukio ambayo wanzanzibari na wasio wazanzibari kuyapiga vita kwa nguvu zote. Binafsi ukizingatia nimefika Zanzibar karibuni, tukio hili limenihuzunisha sana. Kwani si culture ya majority of Zanzibari. Kama unataka Zanziar ibaki na maadili unayotaka wewe, acheni kuwaruhusu watalii kuja Zanzibar. Sifa ya Zanzibar inafahamika na watalii hujiona wana amani wawapo pale. Hawa waliofanya hivi ni watu wachache wanaotaka kuharibia sifa nzuri ya watu na visiwa vya Zanzibar. Nilikuwepo Zanzibar siku za karibuni, na nilijionea mwenye ukarimu wa watu wa Zanzibar ambao hata huwezi kufikiria katika hali ya leo unaweza kukuta watu wastaarabu kama wale. Jambo moja ambalo lilini-touch sana nikiwa na mwenzangu la ukarimu huu tulikuwa tunarudi hotelini jioni baada ya matembezi karibu na muda wa kufuturu. Mzee mmoja alituona na mwenzangu tukiwa tunahangaika kutafuta njia ya kufika kwenye hoteli, pale Stone Town, kwani japo hoteli tulikuwa tukiiona ilee..., lakini vichochoro vya kuifikia tulikuwa hatujavijulia na ilikuwa kama kizungumkuti. Bila kuulizwa, mzee huyu aliyekuwa akipita na zake akiwahi kwenda kufuturu alitufuata na kutuuliza tunaenda wapi, kwani dalili zilionyesha tulikuwa wageni, tukamwambia tunakotaka kwenda. Wala hakuishia kutuelekeza, mzee alituambia nifuateni na akahakikisha tuna fika kwenye mtaa ambao hoteli unaiona straight kwa mbele. Wakati tukitembea kuelekea hotelini , saa hiyo adhana imeshatolewa msikitini na kuashiria kuanza muda wa kufuturu, mita chache mbele tukakutana na jamaa mmoja labda kwenye 30s-40s hivi akiwa anakula tende, tena naye mwenyewe tu, akatuuliza kama tumefunga, na tukamwambia ndio, na akachukua mfuko wote wa tende alizokuwa nazo kashika mkononi na kutupatia ili nasi tuanze kufuturu kwani hatujafika tunakoenda. Natamani kama kungekuwa na watu zaidi kama hawa, tena nyakati zote...
Wewe anon uliyesema hawa vijana walikuwa huko wiki mbili na walikuwa wamekosana na watu mara tatu...naona uwezo wako wa kufikiri ni mdogo, aidha huna elimu na nadhani pia huhitaji kuishi na binadamu. Ina maana ukitofautiana na mtu unamwagia acid ili asione tena? eti kisa ametofautiana na wewe? Kwani kuimba mwezi wa Ramadhani inakatazwa? mbona sijawahi kusikia kuwa inakatazwa? na hata kama inakatazwa watu waambiwe siyo kumwagiwa acid! Waliofanya hivyo hawana elimu ya kuwawezesha kufikiri japo kwa kiwango cha chini sana kama vile pia wanaowatetea hapa. Sidhani hao wanafuata uislaam gani?
ReplyDeletembona hawaonekani kuwa na majeraha ? sura zao ziko kawaida tu? au ni fix ya kuwafanya wazanzibari waonekane maadui mbele ya dunia?
ReplyDelete