Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye tai yenye bendera ya taifa) akimsikiliza Meneja wa Masoko wa Kampuni ya Petra Diamonds Bwana Jeschie Widawski. Balozi Kamala ametembelea Kampuni hiyo leo Antiwerpen Ubelgiji . Kampuni hiyo inauza Almasi kutoka Tanzania.

Bwana Widawski alimweleza Balozi Kamala kwamba kwa mwaka Kampuni hiyo inauza wastani wa crat 20,000 za Almasi yenye thamani ya Dora za Kimarekani millioni 45. 

Aidha, Bwana Widawski alisema Kampuni ya Petra Diamonds baada ya kununua Mgodi wa Almasi wa Mwadui iliwekeza Dora za Kimarekani milioni 45 na imefanikiwa kuongeza ubora wa Almasi inayozalishwa na hivyo kuongeza bei ya Almasi kutoka wastani wa Dora za Kimarekani 90 hadi wastani wa Dora za Kimarekani 250 kwa crat. 

Balozi Kamala ameomba Kampuni hiyo kuongeza uzalishaji na ubora wa Almasi inayozalishwa hili Tanzania iweze kunufaika zaidi na Almasi inayozalishwa Tanzania.

Aidha Balozi Kamala akizunzungumza na wafanyakazi wa Kampuni hiyo alisema yapo mambo muhimu ya kujifunza kutoka Uholanzi katika uendelezaji na usimamiaji wa sekta ya gesi. Uholanzi walipongundua gesi mara ya kwanza katika eneo la Groningen ilikadiriwa kwamba kulikuwa na gesi yenye ujazo wa 2 TCF. Eneo hilohilo baada ya kuanza kuvuna gesi ilibainika lilikuwa na gesi yenye ujazo wa 99 TCF.

Kwa sababu hiyo kiwango cha 43 TCF ambacho kinatajwa kwamba ndicho kimeishagundulika Tanzania, kuna uwezekano mkubwa baada ya kuanza kuvuna kiwango hicho kuongezeka hadi 15,000 TCF ukizingatia uzoefu wa Uholanzi.

Vilevile Serikali ya Uholanzi inapata asilimia 85 ya mapato yote yanayotokana na biashara ya gesi. Kwa sababu hiyo Tanzania lazima tujipange ili tuhakikishe Serikali inapata mapato ambayo hayatapishana sana na Serikali ya Uholanzi inavyopata mapato kutoka kwenye gesi.

Balozi Kamala alisema pia amejifunza kutoka Serikali ya Uholanzi kwamba Serikali inamiliki kwa asilimia zaidi ya tisini miundombinu na biashara ya gesi kwa kutumia Kampuni za Serikali kama vile Gusuine, GasTera na EBN. 

Aidha, Balozi Kamala alisema Serikali ya Uholanzi ina sera mbili zinazoongoza sekta ya gesi ambazo ni sera ya visima vikubwa na sera ya visima vidogo inayotoa fursa ya uwekezaji na uchimbaji wa gesi katika visima vidogo.

Mwisho, Balozi Kamala alimshukuru Bwana Edward Rweyememu wa TANSORT anayefuatilia kwa karibu uuzaji wa Almasi ya Tanzania katika Soko la Almasi la Antiwerpen. Alimweleza kwamba yeye ni jicho la Tanzania na hivyo lazima awe mzalendo na ahakikishe Tanzania inapata mapato yanayotarajiwa kutokana na uuzaji wa Almasi kwa kutumia utaratibu wa tenda.

Aidha, Balozi Kamala ametoa wito kwa Wataalam wote katika sekta ya madini kuwa Wazalendo na wajue Taifa linawasomesha kwa fedha nyingi ili wasaidie Taifa na siku zote waepuke kulipwa na mtu yoyote kwa nia ya kutaka kutoelewa au kuacha kusimamia raslimali za Taifa kwa umakini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. DORA DORA DORA DORA DORA Ndio nini??? Sema DOLA!!! Aghhh unaudhi...

    ReplyDelete
  2. Wayahudi na madini!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...