Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akiwapa nasaha wanamichezo wa wizara hiyo katika tafrija fupi ya kuwaaga wawakilishi wa wizara hiyo ambao watashiriki katika mashindano ya Shirikisho ya Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (Shimiwi) yatakayofanyika mjini Dodoma Jumamosi. Tafrija ya kuwaaga wanamichezo hao ilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Maafisa wa Polisi jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wanamichezo wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi baada ya kuwaaaga rasmi katika tafrija iliyofanyika Chuo cha Maafisa wa Polisi, jijini Dar es Salaam leo. Abdulwakil aliwataka wanamichezo hao wahakikishe wanashirikiana ipasavyo na hatimaye wanashinda michezo aina mbalimbali inayotarajiwa kuanza mjini Dodoma Jumamosi. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...