Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.
Lazaro Nyalandu (Mb) (watano kutoka kushoto msitari wa mbele) akiwa anandamana
pamoja na waandamanaji wanaopinga ujangili wa tembo ‘Tembea kwa ajili ya Tembo’
mara baada ya kuwapokea leo, Ubungo jijini
Dar es Salaam asubuhi. Maandamano hayo yamechukua muda wa siku 19 na
waandamanaji wametembea kilomita 650, kutoka Jijini Arusha.
Matembezi hayo ya kupinga ujangili
yameandaliwa Bw. Patric
Patel, Mkurugenzi, African
Wildlife Trust (wanne kutoka kulia msitari wa mbele) yakiwa na lengo la kuelimisha wananchi
na Ulimwengu mzima kwa ujumla juu ya madhara ya ujangili. Matembezi yamehusisha
raia wa nchi mbalimbali duniani.
Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) ambaye ndiye
mgeni rasmi katika kilele cha matembezi hayo ametoa wito kwa wananchi wote waendelee kushirikiana na serikali kupiga vita
ujangili kwa kuwafichua majangili popote wanapowaona; na taasisi zote za umma
zishirikiane kupambana na ujangili ili kuutokomeza kabisa.
Mkurugenzi wa Idara ya
Wanyamapori, Prof. Alexander Songorwa (aliyeshika
karatasi nyeupe mstari wa mbele) akiwa ameungana na msafara wa waandamanaji eneo la Ubungo kutembea nao
hadi viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo atapokea risala kutoka kwa waandamanaji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...