Meneja wa Magereza Saccos, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza Godfrey Kavishe (wa kwanza kushoto) akiwatembeza Maafisa na Askari toka JKT Saccos katika jengo la Saccos ya Magereza walipotembelea leo Septemba 11, 2013 jijini Dar Es Salaam.
Afisa Mikopo wa Magereza Saccos, Mrakibu wa Magereza Nahman Koko (wa pili kushoto) akiwatambulisha Maafisa na Askari toka JKT Saccos kwa askari Stafu Sajini Naftal Shango(wa kwanza kushoto) anayeshughulika na Usajili wa wanachama walipotembelea Magereza Saccos leo Septemba 11, 2013 jijini Dar Es Salaam.
Meneja wa Magereza Saccos, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza Godfrey Kavishe (katikati waliovaa sare) akitoa maelezo ya utangulizi kuhusu Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara kwa Maafisa na Askari toka JKT Saccos walipotembelea leo Septemba 11, 2013 jijini Dar Es Salaam.
Baadhi ya Maafisa na Askari toka JKT Saccos wakiongozwa na Meja Haule (wa kwanza kulia) wakimsikiliza Meneja wa Magereza Saccos, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza Godfrey Kavishe (hayupo pichani) wakati akitoa maelezo ya utangulizi kuhusu Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara walipotembelea leo Septemba 11, 2013 jijini Dar Es Salaam (Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...