Jumuiya ya Watanzania Sweden, (Tanzaniska Riksförbundet i Sverige),
inawakaribisha Watanzania wote hapa Sweden na nchi za Nordic kushiriki
kwenye mkutano wa majadiliano ya rasimu ya katiba mpya ya Tanzania
utakaofanyika siku ya Jumamosi tarehe 14 Septemba, 2013 kuanzia saa 9 alasiri
(15.00hrs) mpaka 12 Jioni (18.00 hrs) kwenye Ubalozi wa Tanzania, Nasby alle 6,
183 55 Taby.
Majadiliano haya yatasimamiwa na kuendeshwa na Professa Francis
Matambalya wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye kwa sasa yupo Nordic
Africa Institute hapa Sweden.
Hii ni fursa maalum na pekee ya kuwasilisha maoni yenu kuhusu rasimu ya katiba
mpya na majumuisho ya maoni yenu yatawasilishwa rasmi kwa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba mapema wiki ijayo.
Wenye nia ya kushiriki kwenye mkutano huu wanaombwa wathibitishe ushiriki
wao kupitia anwani ya barua pepe tanzanianswe@hotmail.com au kwa ujumbe
mfupi wa simu kwenye namba 0706 50 88 23.
Karibuni sana!
Bi. Seynab Haji
Mwenyekiti wa Muda
Tanzaniska Riksförbunde
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...