Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.

SIKU chache baada ya mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi (MUWSA) kubaini kufanyiwa hujuma ya wizi wa maji katika mitandao yake,mamlaka hiyo sasa imeanzisha operesheni isiyo na kikomo huku ikiwatumia askari polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia(FFU) kusaka wezi hao nyumba kwa nyumba.

Operesheni hiyo imeanza hivi karibuni katika maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi hususani yale yenye viwanda na maeneo yanayokaliwa na watu wa kipato cha juu ambayo yanatajwa kujihusisha na wizi wa maji kwa kujiunganishia kinyume cha sheria.

Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi,John Ndetiko alisema operesheni hiyo imeanza wakati huu ambao kuna upungufu mkubwa wa maji hivyo ufuatiliaji utafanyika katika eneo moja hadi jingine ili kuwabaini wezi wa maji.

“Zoezi hili litakuwa ni endelevu kabisa katika kipindi chote cha uhai wa mamlaka ya maji taka na maji safi mjini Moshi na tumeamua kuianza sasa kutokana na kuwepo kwa upungufu mkubwa wa maji katika maeneo mengi kwa hiyo tutafanya ufuatiliaji katika eneo moja baada ya na jingine ili kuwabaini wanaofanya hujuma hiyo na kuwapeleka kwenye vyombo vya sheria.”alisema Ndetiko.

Akizungumzia kwa nini wameamua kuwatumia askari polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia(FFU)Ofisa uhusiano wa mamlaka hiyo Dorah Kilo alisema sheria za mamlaka zinaruhusu maofisa wake kuingia sehemu yoyote kwa mtu anayetumia maji ama hatumii maji kwa lengo la kukagua miundo mbinu isifanyiwe hujuma.

Alisema kumekuwa na changamoto kubwa ya kiusalama kutokana na maeneo mengine watumiaji wa maji wamekuwa hawatoi ushirikiano kwa kufungua milango yao licha ya kujitambulisha kwao hali inayopelekea kutumia jeshi la polisi pamoja na viongozi wa mitaa husika.

“Mara nyingi tunatangulia sisi wenyewe katika eneo husika,tunakuja kirafiki tunazungumza ili kuweza kutambua matatizo yako na kasha kuchukuliwa hatua, lakini unapokuwa unaleta ugumu wa kutoa ushirikiano pale ndipo tunalazimika kuwaagiza askari polisi kuja kuongeza nguvu.”alisema Killo.

Alitoa wito kwa wakazi wa mji wa Moshi na maeneo mengine yanayosimamiwa na mamlaka hiyo kutoa taarifa za hujuma ya maji katika maeneo yao na kwamba atakayotoa taarifa sahihi ya wizi huo atazawadiwa na mamlaka hiyo kiasi cha fedha ambazo hata hivyo hakukitaja.
Baada ya kusimama muda mrefu baadhi ya watu waliokuwa wakishuhudio tukio hilo la kutafuta maungio ya maji walilazimika kunywa maji yale yale yaliyoungwa kwa wizi.
Sehemu ya mauongio ya maji katika njia kuu ya maji iliyopita ndani ya eneo hilo.
Baada ya kusimama muda mrefu baadhi ya watu waliokuwa wakishuhudio tukio hilo la kutafuta maungio ya maji walilazimika kunywa maji yale yale yaliyoungwa kwa wizi.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Wizi namna yeyote wa mali ya uma unakera sana.Naona jamaa watumia polisi na kadhalika kuwasaka hao wizi, naona wanapotesa wakati. Mimi nina njia rahisa sana ya kukomesha wizi huo, nao waja kwa matawi matatu.
    1. General AMNESTY, yaani wizi wote wasamehewe kwa muda wa miezi mitatu hivi,na wakati huo waende wenyewe kujisalimisha na kujisajili and no back payment.
    2. Baada ya miezi hiyo ya amnesty, nyumba yeyote itakayokamatwa na wizi ikamatwe na uma,CONFISCATED na iuzwe na pesa zitiwe kwenye hazina ya nchi.
    3.Draconian law ipitiswe kuwa atakaye kata rufaa, akishindwa, nyumba yake ichukuliwe naye akasote jela.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...