Leo tarehe 12 Septemba 2013, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewatembelea wajasiliamali, Raia wa Tanzania wanaoishi na kufanya shughuli zao nchini Zambia katika maeneo ya viwanja vya COMESA. Katika zaira hiyo iliyofana, Mhe. Naibu Waziri aliambatana na Mhe. Grace Mujuma, Balozi wa Tanzania nchini Zambia pamoja na maofisa wengine wa Wizara ya Mambo ya Nje.
Baada ya kutembelea mabanda mbalimbali na kukagua shughuli zinazofanywa na Watanzania hao, Mhe. Naibu Waziri alipata fursa ya kubadilishana nao mawazo. Watanzania hao walielezea furaha yao kwa kutembelewa na kiongozi wa Serikali ya Tanzania na kubainisha kufarijika kwao kwa namna Serikali yao inavyowajali.
Waliomba juhudi zifanyike kupanua barabara katika eneo la Tunduma ili kupunguza msongamano wa magari katika eneo hilo. Aidha, waliomba mashauriano yafanyike ili kituo cha mpaka cha Tunduma/Nakonde kifanye kazi kwa masaa 24. Walisema hatua hiyo itasaidia kuondoa msongamano, kuongeza kasi ya biashara, kupunguza vitendo vya jinai na kuiongezea mapato Serikali.
Naye Mhe. Naibu Waziri aliwapongeza Watanzania hao kwa kuamua kufanya shughuli zinazoweza kuwapatia kipato cha halali na kujenga taifa lao. Aliwataka wahakikishe kwamba wote wanaishi kisheria na kufuata taratibu zilizowekwa na mamlaka za Zambia ili kuepusha usumbufu kwao na kwa Serikali. Aidha, aliwataka wasijihusishe na vitendo vyovyote vya jinai ili kuepusha kuchafua sifa nzuri za taifa la Tanzania.
Mhe. Naibu Waziri yupo nchini Zambia akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa kimataifa kuhusu Mkataba unaolenga Kutokomeza matumizi ya Mabomu ya kusambaa (Convention on Cluster Munitions). Kabla ya kutembelea wajasiri-amali, Mhe. Najbu Waziri alikutana na kuzungumza na Watanzania wa rika na kada mbalimbali wanaoishi nchini Zambia, mazungumzo ambayo yalifanyika katika Ubalozi wa Tanzania, Lusaka.
Mhe. Naibu waziri akikagua shughuli za wajasiriamali Watanzania katika soko la Comesa. Wa kulia kutoka alipo Naibu Waziri ni Mhe. Grace Mujuma, Balozi wa Tanzania nchini Zambia na wa kulia ni Bw. Mboweto, Raia wa Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Soko la Comesa.
Kama mtaa wa kongo zamani,au mnadani kariakoo
ReplyDeleteSi watatimuliwa kama walivyowatimua wenzao huku.
ReplyDelete