Marehemu Adubo Mustafa Omer 
enzi za uhai wake

Baada ya uchunguzi wa zaidi ya wiki tatu,Ubalozi wa Tanzania Washington DC umethibitisha kuwa Marehemu Adubo M. Omer hakuwa Raia wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania bali alikuwa Raia wa Sudan.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa Idara ya Uhamiaji Makao Makuu Dar Es Salaam ilielezwa kuwa,hakuna kumbukumbu zozote zinazoonyesha kuwa, Marehemu Adubo aliwahi kupewa Uraia wala Pasipoti ya Tanzania.
Aidha,kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa kutoka kwenye taasisi mbali mbali za Kiserikali zilizopo mjini Dallas Texas, Marehemu Adubo M Omer alizaliwa tarehe 25.04.1956 katika sehemu iitwayo Maridi Abang, iliyopo Sudani ya Kusini.

Taarifa zaidi zinaonyesha kuwa marehemu Adubo, alikuwa amepewa hati ya kudumu ya ukaazi Nchini Marekani (Permanent Resident card) ambayo ilikuwa inamaliza muda wake tarehe 8.03.2014.

Ubalozi ulipotaka kujua, ilikuwaje hadi ofisi ya 'Medical Examiner' ambayo inafanya uchunguzi wa sababu za kifo cha Marehemu Adubo imtambulishe ubalozini marehemu huyo kama Raia wa Tanzania? Msemaji wa ofisi hiyo alieleza kuwa, hii ni kwa mujibu wa maelezo ambayo marehemu mwenyewe aliyatoa kwenye kituo cha Police cha Dallas, alikokuwa amekamatwa na
kuwekwa ndani kwa siku chache kisha akaachiwa kabla ya kifo chake.

Inaelekea Marehemu Adubo hakutaka Uraia wake ujulikane kwa sababu ambazo hazikuweza kueleweka. Suala hili, lilileta utata na hisia ambazo zimeuletea Ubalozi usumbufu ambao haukuwa na ulazima wowote.

Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania washington DC, inapenda kuwashukuru Watanzania wote waliopo Ndani na Nje ya Nchi waliosaidia katika jitihada za kupatikana kwa taarifa sahihi za mtu huyu. vile vile Ubalozi unazishukuru taasisi zote za hapa Marekani ambazo kwa namna moja au nyingine zimetoa ushirikiano wenye tija uluotuwezesha kulitatua suala
hili.

Shukurani za pekee, ziwaendee blogs za vijimambo na swahili villa, bila kuwasahau uongozi wa jumuia ya Watanzania waishio Dallas Texas, Bw Franklin Maji, Mchungaji Absalom na Bi aysha Burnett.
                  IMETOLEWA NA OFISI YA UBALOZI WA TANZANIA
WASHINGTON DC.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Atakuwa mbongo huyo, ila ili apate uraia wa Marekani kama mkimbizi lazima alidanganya ni Msudani kusini. Ni janga kwa kweli

    ReplyDelete
  2. Ni kweli mdau wa kwanza, inawezekana kabisa jamaa ni mbongo, maana wabongo wengi tu (especially ambao hawajapita shule) wamejilipua huku ughaibuni na mara kwa mara wanajifanya wanatoka kwenye nchi ambazo zina vita ect, wapo wabongo wanyarwanda, Burundi, wa sudani, sasa inapofika majangwa kama haya basi wanakuwa wanatelekezwa, it is a sad end indeed, labda kama ana ndugu wanaosoma globu ya jamii wamtambue, lakini kama makaratasi yanasema ni msudani, then hard luck, RIP.

    ReplyDelete
  3. Mh mdau hapo juu umechanganya mambo! angekuwa mbongo wangeona uhamiaji Tz ambako uchunguzi ulifanyika na USA. Huyo hakuwa mtanzania mie nilicomment tangu wamemuweka mwanzoni kuwa ndugu zake wajitokeze, niliona hata hilo jina mashaka matupu Adubo! Kumbe ni kweli sio Mtz. watu wa mataifa mengine wakiwa nje wanapenda kujisingizia ni watanzania shauri watanzania wanajulikana kuwa ni watiifu, waaminifu, ni watu wazuri sana. Ila kwa sasa na hilo sembe sijui tunaonekanaje???????Mungu ibariki Tanzania na watu wake.

    ReplyDelete
  4. Mh mdau hapo juu umechanganya mambo! angekuwa mbongo wangeona uhamiaji Tz ambako uchunguzi ulifanyika na USA. Huyo hakuwa mtanzania mie nilicomment tangu wamemuweka mwanzoni kuwa ndugu zake wajitokeze, niliona hata hilo jina mashaka matupu Adubo! Kumbe ni kweli sio Mtz. watu wa mataifa mengine wakiwa nje wanapenda kujisingizia ni watanzania shauri watanzania wanajulikana kuwa ni watiifu, waaminifu, ni watu wazuri sana. Ila kwa sasa na hilo sembe sijui tunaonekanaje???????Mungu ibariki Tanzania na watu wake.

    ReplyDelete
  5. Mdau wa Kwanza, kwa jina na sura huyo si Mtanzania!

    Tunajuana na raghba zetu kuanzia Makabila na tabia zetu sisi Watanzania.

    Ofisi ya Ubalozi ina Mafisa wana uzoefu mkubwa sana na ulelewa kuhusu masuala yahayohusu watu na mabmbo kama hili, hivyo Uchunguzi wao huwa unazama kwa kina kabla hawajatoa Kauli, hivyo Mdau tafadhali usiwashushe uwezo Maafisa wetu wa Ubalozi hapo Washington-DC, wamefanyia kazi hili suala kwa umakini mkubwa kabla hawajatoa tamko.

    Ndugu zetu Waafrika wenzetu wanautumia Uraia wetu wa Tanzania vibaya!, hebu angalia jamaa anakamkatwa KWA MAKOSA ANAFIKA POLISI anakana Uraia wake halali anataja yeye ni Mtanzania!

    ReplyDelete
  6. Kumbukeni ''OPERESHENI KIMBUNGA Tanzania''!

    Ndugu zetu Majuu muangalie sana kudanganya danganya kutawaponza!

    Kazi kwenu Majuu ndugu zetu kwa kudanganya Uraia wenu halali!

    Wewe unadanganya kua wewe ni Mrundi ukiwa Majuu ili upate Ukimbizi, matokeo yake hadhi ya Ukimbizi inakwisha unarudishwa Burundi ukifika unatupwa Bongo na Bongo unakumbana na ''OPERESHENI KIMBUNGA'' unamwagwa tena Bujumbura Burundi na Dk.Emmanuel Nchimbi na Vijana wake wa Uhamiaji, je utamlaumu nani?

    ReplyDelete
  7. Kama Uraia ataukosa kiwa Marehemu aliyetangulia mbele za haki, mtendeeni haki angalau mumzike.

    Watanzania mzikeni kama Mwanandugu Mwafrika mwenzetu!

    ReplyDelete
  8. HUYU NI MTANZANIA KABISA AMBAYE ALIITUMIA SUDAN ILIAWEZE KUPATA UKAAJI WA HAPA.MIMI MWENYEWE NI MTANZANIA HALISI LAKINI PIA NIMEANDIKA NIMEZALIWA SUDAN NANIMEPATA KIBALI CHA KUISHI HAPA.

    ReplyDelete
  9. Anaweza kuwa mtanzania sasa hao ubalozi na uhaniaji Tanzania wamemtabua kwa jina gani ?kama amebadili jina watajuaje? Ukweli anao marehemu mwenyewe kazi kweli kweli. Makaratasi hayo

    ReplyDelete
  10. Wewe uliyeongelea kuhusu jina ya kuwa linaonekana si la TZ...Wakeup!!!
    Dont judge the book by the cover...
    What is jina??? A name can be anywhere, in fact huko East Africa ni very mixed place. It is difficult to differenciate nani asili yake ni wapi. Mimi naishi huku majuu, asilimia ya watu wengi ninaokutana nao wanasema mimi ni Mganda au wakati mwingine wanafikiri ni Mkenya. Haya mambo ya kujipa uraia wa nchi za watu na kujipa uraia wa nchi za watu ili kurahisisha maisha huku majuu ni kitu cha kawaida hata wakuu wa nchi husika hilo wanalijua. Kuhusu marehemu kikubwa ni kutafuta jamaa zake kupitia njia mbalimbali. Jina sio issue

    ReplyDelete
  11. Huyu jamaa aliomba ukimbizi tu kama msudan lakini huyu ni mbongo kabisa tena ni msukuma huyu....mzikeni tu maiti haina kabila wala nchi jamani

    ReplyDelete
  12. Hivi vibali pamoja na kulizimisha kuishi nchi za watu vinatufanya tujirudishe kule kule ktk enzi za utumwa !!!
    Sasa wewe ni mtanzania kwa sababu tu ya kujiendeleza ubishi majuu unabadilika kuwa mrundi au msudani huu kama si iTunes ni nini, Haya sasa mauti yako kukuta shida ndiyo hiyo !! Inatoa huruma kwa kweli. Bora maskini Hutu kuliko Tajiri mtumwa

    ReplyDelete
  13. KUNA MTU AU BALOZI YETU IMETOA TAHARIFA KWA UBALOZI AU JUMUIA YA SUDAN ILI BINADANU MWENZETU APATE KUHIFADHIWA KWA UTU? YOTE NI KATIKA HARAKATI ZA MAISHA. KUNA RAIS WA TAIFA KUBWA AMBAYE MPAKA LEO WANAWASI WASI NAYE KWAMBA SI MWENZAO. KENETH KAUNDA ALUTIMULIWA ZAMBIA KWAMBA SIO RAIA MWENZA. NI VISA TU VYA DUNIA HII YETU WOTE NA WALIMWENGU WAKE BAGUZI.

    MUNGU ATUBARIKI ZAIDI

    Ameen

    ReplyDelete
  14. HUYU MTU MIMI NINAHAKIKA KABISA NI HANCE KAPELA ALIKUWA ANAFANYAKAZI WIZARA YA NISHATI MWADUI SHINYANGA.WEKENI PICHA ZAKE KWENYE MAGAZETI YA NYUMBANI WATAMTAMBUA.JAMAA KATOKA NYUMBANI NI MIAKA KARIBU 30 KWA SASA.MDAU SWEDEN.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...