Na Mashaka Mhando
BENKI ya NMB imetoa mafunzo ya wiki mbili kwa vyama vya ushirika vya wakulima wa mpunga na SACCO'S wilayani Korogwe, mafunzo yaliyolenga kuwaongezea uwezo wa namna watakavyoweza kuviendesha vyama hivyo katika dhana nzima ya kuondoa umasikini kwa wanachama wao.
Mafunzo hayo ambayo yalikuwa yakitolewa na mkufunzi wa mafunzo hayo Bw. Alfred Chonya yalianza tangu Agosti 17 mwaka huu na kufungwa Septemba 3 na Mkuu wa wilaya ya Korogwe Bw Mrisho Mashaka Gambo kwenye aliyofanyika kwenye ukumbi wa Matunda katika mji mdogo wa Mombo wilayani Korogwe.
Akizungumza katika mafunzo hayo Bw Gambo alisema ni ushahidi uliokuwa wazi kwa benki ya NMB ambayo imekuwa ikifadhili miradi mbalimbali katika wilaya hiyo kila inapoombwa hivyo mafunzo wanayotoa kwa wana-ushirika yatasaidia mbinu bora na uelewa wa namna kuendesha vyama hivyo vya ushirika kutokana na kwamba mara nyingi kumnekuwa na matatizo.
"Kazi ya kutoa elimu ilikuwa itolewe na serikali kupitia maofisa ushirika waliopo, lakini wenzetu wa NMB kwa kujali namna ya kushirkiana na wateja wao, wameonelea ni vema wakatoa mafunzo haya, kwa niaba ya serikali tunawapongeza na tunawaomba muwe na moyo huo wa kuwasaidia wateja wenu,"alisema.
Alisema serikali kuanzisha ushirika lengo lake lilikuwa kuwakomboa wakulima na wana-ushirika mbalimbali hivyo suala la NMB kutoa mafunzo hayo kutakuwa ni ukombozi mkubwa ingawa alisema mara nyingi mafunzo huwa yanatolewa kwa viongozi wa ushirika akaonesha haja ya wakati mwingine ni vema wanachama nao wakafaidika na mafunzo ya namna hiyo.
Bw. Gambo alisema serikali ina nia njema ya kuwasaidia wajasiriamali wadogo ili waweze kujikwamua kiuchumi na suala la benki ya NMB kusaidia vikundi hivi katika wilaya yetu ni jambo la faraja kubwa kwa sababu litawafanya waweze kuendesha vikundi vyao kwa utaalamu na umahiri wa kufunga mahesabu na kukopa kwa makini na marejesho yake.
Awali mkufunzi wa mafunzo hayo Bw. Chonya ambaye alisema mafunzo hayo wameyatoa kupitia idara mpya ya NMB ya maendeleo ya Kilimo (NFAD) 'Foundation For Agricultural Development', alisema vikundi mbalimbali walivyowapa mafunzo waliweza kuwafundisha wajibu wa bodi za mikopo, wajibu wa katibu au meneja wa sacco's, Misingi ya Utawala Bora, Sifa ya kiongozi wa bora na wajibu na haki kwa wanachama.
"Tumeweza kuwapa mafunzo haya katika ngazi mbalimbali kwa mfano unaposema sifa ya kiongozi bora ni ipi ni lazima awe mkweli daima, huongoza kwa kuonesha njia na pia awe anafuata misingi ya utawala bora kwa kuwa mwanimifu kwa wenzake na yale anayoyafanya," alisema Bw Chonya.
Meneja wa NMB tawi la Korogwe Bw Erasto Mwamalumbili, alisema benki hiyo imeanzisha idara hiyo mpya kwa lengo la kuwafuata wananchi kule walipo hasa katika maeneo ya vijijini kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kukopesheka kwa ajili ya kuongeza mitaji yao ya kilimo na vyama vyao vya ushirika.
Alisema baada ya mafunzo hayo ya awamu ya kwanza wanatarajai watatoa tena mafunzo ya awamu ya pili ili waweze kuwasaidia wakulima na vyama vya ushirika vilivyopo katika wialya hiyo ya Korogwe.
Akitoa shukurani zake Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini Bw Stephen Ngonyani 'almaarufu Profesa Majimarefu', alishukuru benki hiyo akieleza kwamba imekuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi hasa waliokuwa vijiji na kwamba atakuwa balozi wao bungeni kwa kuishawishi serikali itazame kwa jicho la pekee kwa vile imekuwa ikiwasaidia mno wakulima na wananchi kwa ujumla wenye kipato cha chini.
Wanachama wa sacco's wakisikiliza kwa makini ufungaji huo.
Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini Bw Stephen Ngonyani 'almaarufu Profesa Majimarefu', akichangia neno la shukurani
Mwenyekiti wa Chama Cha mapinduzi CCM, Bw Nassoro Hemed 'Malingumu' (shoto) akimpongeza meneja wa benki ya NMB tawi la Korogwe Bw Mwamalumbili kuhusu namna alivyoweza kuwaasaidia wajasiriamali wadogo kwa mikopo ya JK.
Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mhe. Mrisho Gambo akizungumza wakati akifunga mafunzo hayo.
Picha ya pamoja ya viongozi wa NMB kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya korogwe,
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...