Wachezaji wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) wamerejea nyumbani baada ya mechi yao na Gambia ambapo walifungwa 2-0 huku matarajio yote sasa yakiwa ni kufuzu kucheza Kombe la Afrika 2015.

Wachezaji hao 18 pamoja na benchi la ufundi waliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere saa nane mchana kwa ndege la shirika la Kenya.

Hii ni mechi ambayo Taifa Stars, inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, ilitakiwa kushinda lakini ilikosa wachezaji tisa muhimu ambapo baadhi yao hawakuruhusiwa na vilabu vyao na wengine walikuwa majeruhi.

Akizungumza baada ya kuwasili kocha Kim Poulsen alisema kuutkana na hali halisi alilazimika kuwachezesha wachezaji vijana ambao uzoefu wao sio mkubwa sana kama ule wa wachezaji wa kawaida ambao mara nyingi huwa wanaanza.

“Tumesikitishwa na matokeo haya lakini kama nilivyosema Gambia waliita wachezaji wao wote wanaocheza nje lakini sisi tulikosa timu karibu nzima….vijana waliocheza walijitahidi lakini wenzetu waliwazidi uzoefu,” alisema.

Alisema ni muhimu watanzania watambue kuwa mechi za kufuzu kucheza kombe la dunia zimekuwa muhimu sana kwa Tanzania kwani wachezaji wengi wametambulika na wameitwa nje. “Kuna wachezaji kama Shomari kapombe, Mwinyi Kazimoto, ambao kutokana na mechi hizi wamepata nafasi ya kwenda kucheza nje,” alisema.

Kocha huyo alisema yuko makini sana kutekeleza mpango wa muda mrefu ambao ni kuhakikisha Tanzania inafuzu kucheza Kombe la Afrika 2015,” alisema na kuongeza kuwa timu anayoendelea kujenga itafanya kazi hiyo.

Alisisitiza kuwa ni lazima TFF ihakikishe wachezaji wote muhimu wanakuwepo wakati mechi za kufuzu kucheza Kombe la Afrika zitakapoanza mwakani.

“Kwa sasa wachezaji watarudi vilabuni kwao na baada ya muda mfupinitawaita tena ili tujiandae na Mashindano ya CECAFA Senior Challenge yatakayofanyika Nairobi,” alisema.

Aliwataka watanzania wawe na subira kwani ana imani na timu anayoijenga.

Akiunga mkono maneno ya Poulsen, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe, ambaye bia yake inadhamini Taifa Stars, alisema ni lazima nguvu zote zielekezwe katika AFCON 2015.

“Tungefurahi kama tungefuzu kucheza Kombe la Dunia lakini ni mapema sana kwa timu yetu ambayo bado inajengwa…tumpe kocha nafasi aweze kutimiza haya malengo na sio kumkatisha tama,” alisema.

Alisema wao kama wadhamini wanafarajika na mabadiliko mbalimbali yaliyofanyika katika Timu ya Taifa tangu waanze kuidhamini Timu hiyo mwezi Mei mwaka uliopita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Ni kati ya mechi mbaya ambazo Taifa S.imewahi kucheza.Balaa limeanza walipoamua kupanda boti kuingia Gambia ,pesa za tiket kwa ndege hazikutosha?au ziliota miguu.
    Wachezaji 9 wazuri hawakuruhusiwa na klabu zao,Hiyo itawezekanaje,kwa nini viongozi wa Taifa Star wasikubaliane na viongozi wa klabu za hao wachezaji,au kwa nini wapanga ratiba ya ligu kuu ya Bongo wasiangalie ratiba ya mashindano kombe la dunia kwani hapa Ulaya ligi zote sasa ziko likizo kwa 14 days.Sasa kwa nini hata sisi tusifanye vile kuwezesha wachezaji wote wa Taifa Star waende wakatetee uzalendo wao? Je kuna tofauti gani kubadilisha jina na kuitwa Kilimanjaro Star kama viongozi na wachezaji ni walewale na mawazo yao ya kienyeji enyeji na kuiba pesa za walipa kodi
    . Inabidi kuwauliza ziko wapi pesa za tiket ya ndege walizotakiwa waende hadi Banjur? Hivyo basi napendekeza.
    1.Kocha mpya ili aunde timu mpya ya Taifa.
    2.Iundwe kamati ya kuchunguza ubadhilifu wa pesa za serikali ndani ya taifa Star.
    La sivyo hata hayo mashindano yajayo tutakuwa Wasindikizaji Star.

    ReplyDelete
  2. yaani hawa wamefungwa wanacheka cheka tu. Wanaona poa, duh!

    ReplyDelete
  3. Hayo maneno ya kocha hayana mshiko, kwani wachezaji wote wanaoitwa Taifa Stars wanatakiwa wawe wazuri, kukosekana baadhi sio maanake wafungwe na timu dhaifu kama hiyo.Dawa:
    1.Ifumuliwe kamati ya ufundi yote ichagkuliwe mpya, wayolewe wote wakina pondamali, Mukebezi, Marsh, n.k.Maana hao ndio wanamshauri kuchagua wavhezaji wa DSM tu badala ya kwenda mikoani na kutafuta wachezaji.kwa mfano kocha anamchaguaje Henri Joseph wakati hajamuona kiwango chake, kwa nini anamg'ang'ania Erasto Nyoni wakati hajavheza ligi na ni mbovu na ametufungisha mechi karibu nne zilizopita.
    2:Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Sunday Kayuni afukuzwe atafutwe mtu makini.Watu wavisahau hibyo vyeo wanamuangalia kocha tu.Mkurugenzi wa ufundi ni cheo muhimu sana, Kayuni amekaa karibu miaka kumi na hamna maendeleo yeyote ya Taifa Stars pamoja na udhakini mkubwa, hivyo abadilishwe.
    3.kivunjwe kikosi cha Taifa Stars kiundwe upya kwa kutafuta wachezaji nchi nzima,
    4:Ikiwezekana atafutwe kocha mwingine maana huyu amefungwa mevhi sita mfulilizo wachezaji hawawezi kumuheshimu.Tusipotimiza hay Timu yetu haiendi kokote.

    ReplyDelete
  4. kwa nini tusicheke ikiwa sisi(wasindikizaji Star-kama ilivyosema hapo juu) na viongozi tumepata chetu.Hakuma tulichopoteza,talking talking zenu kesho you sleep.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...