Kikosi cha Tanzania
mchezaji wa timu ya Ghana, Michael Owusu akimkabili mchezaji wa timu ya Tanznia wakati timu hizo zilipochuana vikali katika michuano ya Afrika ya Airtel Rising Stars iliyofanyika uwanja a Onika Lagos Nigeria
Mchezaji kiungo wa timu ya Tanania George Emmanuel akikabiliwa na mchezaji wa timu ya Ghana wakati nchi hizo zilipopambana vikali katika mechi za michuano ya Afrika ya Airtel Rising Stars iliyofanyika uwanja a Onika Lagos Nigeria Ghana ilishinda 2 - 1.

Jumanne September 17 2013.. Tanzania imeanza vibaya mashindano ya kimataifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars baada ya leo kukubali kipigo cha goli 2-1 dhidi ya Ghana. Mechi ya wasichana inatarajiwa kupigwa baadae leo ambapo watakutana na Sierra-Leone.

Mashindano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars yanafanyika kwa mara ya pili, kwa mara ya kwanza yalifanyika nchini Nairobi na Niger kuibuka mabingwa , lengo la mashindano haya ni kuzalisha vipaji vingi vya timu za taifa barani Afrika. Katika mechi ya leo , Tanzania ilikua ya kwanza kupata goli katika dakika ya 26 kupitia kwa mshambuliaji hatari Athanas Mdam baada ya kuwapiga chenga mabeki wa Ghana.

Ghana walifanya shambulizi la hatari na kupata goli la kusawazisha katika dakika ya 30 kupitia kwa Prince Agyeman baada ya kuwazidi mbio mabeki wa Tanzania na kuachia shuti kali lilimzidi mlinda mlango wa Tanzania.

Juhudi za Tanzania kupata goli la pili hazikuzaa matunda , dakika ya 45 kipindi cha kwanza Ghana waliongeza bao la kuongoza na lililodumu mpaka kipyenga cha mwisho kupitia kwa Godfrey Nyarko baada ushirikiano mzuri wa washambuliaji wa Ghana.

Timu ya wavulana ambayo ipo kwenye kundi D pamoja na Ghana , Zambia , Sierra-Leone itacheza mechi ya pili dhidi ya Zambia jumatano sembemba 18 , watamaliza na Sierra –Leone katika mchezo wa mwisho wa makundi.

Timu ya wasichana , baada ya kucheza na Sierra –Leone watakutana na Uganda jumatano , Septemba 18 kabla ya kukutana na Malawi siku ya Alhamisi , September 19. Mashindano yanaingia hatua ya mtoano ijumaa na fainali itapigwa jumapili , Septemba 22.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...