Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania kiwanda cha Mbeya wamehitimisha shamrashamra za kupokea udhamini wa Castle Lager kwa FC Barcelona zilizodumu kwa mwezi mmoja nchi nzima. Kama ilivyokuwa maeneo mengine, maelfu ya mashabiki wa soka jijini Mbeya pia wamepata fursa ya kuwa sehemu ya shamrashamra hizo zilizofanyika mwishoni mwa wiki na kuvutia maelfu ya mashabiki wa kandanda.

Shamrashamra hizo zilihusisha maandamano makubwa ya wafanyakazi wa Kampuni Bia Tanzania (TBL) pamoja na vikundi vya sanaa vya Magereza Brass Band na Bombeso waliokatiza katika mitaa ya jiji la Mbeya wakitoa burudani ya muziki, matarumbeta na manjonjo ya kucheza kandanda.

Wakati wa maandamano hayo mashabiki wengi wa mpira wa miguu walijitokeza barabarani kushuhudia utambulisho huo, baadhi yao wakiwa wamevalia jezi za Barcelona.

Maandamano hayo yaliyowahusisha wafanyakazi wa TBL yalianzia katikati ya jiji la Mbeya na kupita katika mitaa kadhaa ya katikati ya jiji la Mbeya na kuishia Iyunga kilipo kiwanda cha TBL yakiwa na lengo la kuutambulisha ubia wa Castle Lager na Barcelona kwa wafanyakazi wa TBL pamoja na wadau wa michezo wa Mbeya.

Pia maandamano hayo yalikuwa na lengo la kuonyesha sapoti ya wafanyakazi hao kwa ubia wa Castle Lager na FC Barcelona, ambayo inatajwa kuwa ni klabu ya karne kutokana na mafanikio makubwa na kuwa na wapenzi wengi zaidi duniani kuliko timu nyingine yoyote.

Wakati wa maandamano hayo mashabiki wengi wa mpira wa miguu walijitokeza barabarani kushuhudia utambulisho huo, baadhi yao wakiwa wamevalia jezi za Barcelona.

Akizungumza na wafanyakazi wa TBL katika hafla iliyofanyika kwenye kiwanda cha TBL Mbeya kuhusu ubia wao na Barcelona, Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa TBL, James Kavuma amesema wafanyakazi wa TBL Mbeya na wananchi wa Mbeya wameupokea udhamini huo kwa furaha kwani anaamini kuwa udhamini huo utaweka karibu mashabiki wa Barcelona na klabu yao waipendayo kupitia bia ya Castle Lager.

‘’Udhamini huu umelenga mambo mengi, moja ikiwa ni kuwaweka karibu wapenzi wa klabu hiyo waliopo Tanzania na Barcelona. Lakini si hilo tu, yapo mambo mengi yenye manufaa kwa jamii yatakayopatikana kutokana na udhamini huo wa miaka mitatu.’’

Naye Meneja Mauzo wa Kanda hiyo, Michael Myinga alisema kuwa kutokana na historia ya zaidi ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa FC Barcelona na Castle Lager basi ubia huu unaleta maana kubwa na ni muafaka ukizingatia kuwa Castle Lager ni kinywaji cha bara zima la Afrika.

Meneja wa Castle Lager Kabula Nshimo alisema kwamba sherehe hizo zilizofanyika Mbeya ndio za mwisho katika mlolongo wa kuzindua mahali pote ambapo TBL ina viwanda. Aliongeza kuwa sasa shughuli nyingine mbalimbali zinazohusisha wadau wa soka na jamii kwa ujumla ndio zitakazofuatia kupitia shughuli mbalimbali zilizopangwa kufanyika nchi nzima katika.
Wafanyakazi wa TBL Mbeya wakicheza kwaito kusherekea udhamini wa Castle Lager kwa FC Barcelona.
Wafanyakazi wa TBL Mbeya wakicheza foosball kusherekea udhamini wa Castle Lager kwa FC Barcelona.
Wananchi wa jiji la Mbeya wakitazama maandamano ya wafanyakazi wa TBL Mbeya kupokea udhamini wa Castle Lager kwa FC Barcelona.
Wafanyakazi wa TBL Mbeya wakicheza mduara kusherekea udhamini wa Castle Lager kwa FC Barcelona.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...