Kikosi cha timu ya wavulana kinachoshiriki michuano ya Airtel Rising stars nchi Nigeria wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuondoka katika uwanja wa Julius Kambarage nyerer kuelekea Nigeria kwenye michuano ya Afrika inayoshirikisha timu kutoka nchi 17 barani Afrika .Wa kwanza kulia ni mwakilishi wa Airtel Bi Lilian Kibiriti
Kikosi cha timu ya wasichana kinachoshiriki michuano ya Airtel Rising stars nchi Nigeria wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuondoka katika uwanja wa Julius Kambarage nyerer kuelekea Nigeria kwenye michuano ya Afrika inayoshirikisha timu kutoka nchi 17 barani Afrika. (mwenye shuti) ni kocha wa timu hiyo Rogacian Kaijage.
Kikosi cha timu ya Airtel Rising stars wakati wa ufunguzi wa michuano ya Airtel Rising Stars ya Afrika inayozinduliwa rasmi jana (jumatatu) Nchini Nigeria na kushirikisha timu kutoka katika nchi 17 barani Afrika.

Timu zinazoshiriki michauano ya pili ya Afrika ya Airtel rising Stars inayofanyika nchini Nigeria mwaka huu zimewasili ambapo michuano hiyo imeanza rasmi jana katika viwajnja vya Agege. michuano hiyo imeudhuriwa na wachezaji guru wakiwemo Rober Pires mchezaji nyota wa zamani wa kablu ya Arsenal

Timu ya Zambia ilikuwa yakwanza kutua siku ya Ijumaa ikifatiwa na timu ya Ghana iliyotua muda mchache baadaye siku hiyo. timu ya mabigwa watetezi kutoka Niger ilitua katika uwanja wa ndege wa Murtala Mohammed International siku ya jumamosi mchana pamoja na timu kutoka Congo Brazzaville

kikosi cha timu ya Tanzania kiliwasili siku ya jumapaili chini ya kocha Abel Mtweve na timu nyingine zinategemea kuwasili kabla ya michuano hiyo kuanza siku ya jumatatu

michuano ya Airtel Rising stars ni michuano ya kipekee ya nchi za Afrika yenye lengo la kuvumbua na kukuza vipaji huku ikiwezesha nchi za Afrika kupata wachezaji wa timu za taifa

kwa kupitia mashindano haya Airtel inatoa nafasi kwa vijana hawa kutimiza ndoto zao, na kuonyesha uwezo wao kwa zaidi ya mamilioni ya watu alisema mkurugenzi mkuu wa Airtel Nigeria bwana Segun Ogunsanya

aliongeza "wachezaji wengi wameshiriki michuano mikubwa kama hii kwa mara ya kwanza na wanafurahia kupata nafasi ya kushindana na wachezaji nyota wengine toka katika nchi mbalimbali. kwa wiki nzima tunaamini wachezaji hawa watabaki na kumbukumbu ya mpira ambayo wataifurahia katika maisha yao siku zote"

michuano ya Airtel Rising stars itafanyika nchini lagos Nigeria kuanzia tarehe 16 hadi 22 septemba 2013. wachezaji nyota waliochaguliwa watashiriki katika clinic itakayosimamiwa na makocha wa Manchester united inayotegemea kufanyiaka mwaka kesho April 2014 nchini Lubumbashi (Democratic Republic of Congo).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Jamani Jamani angalieni bendera ya taifa inavyofanywa,hivi hadi leo waTanzania hatujui bendera yetu inakaa vipi,hebu angalieni picha hizo muone,Bendera ya Taifa imegeuzwa kichwa chini miguu juu

    ReplyDelete
  2. Kwa namna mlivyobeba bendera ya taifa Mhmm!!Ila ni matumanini yangu mtafanya vizuri,na kuiletea nchi yenu sifa.

    ReplyDelete
  3. Hawa jamaa vichwa bovu kabisa. hata namna ya kubeba bendera hamjui..mliwezaje kufika huko....AIBU TUPU

    ReplyDelete
  4. Inasikitisha kuona vijana wetu hawajui namna bendera yetu inavyotundikwa au kubebwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...