Sayansi maana yake ni maarifa . Tunapo zungumzia dhana ya sayansi ya kiafrika , tunakuwa tunamaanisha matumizi ya maarifa ya kiafrika katika kukabiliana  na mazingira ya mwanadamu pamoja na changamoto mbalimbali zinazo mkabili .

Tafiti mbalimbali za ki akiolojia na ki-anthropolojia zinaonyesha kuwa sayansi ya kiafrika imekuwapo kwa takribani miaka bilioni mbili sasa, hii  ikiwa na maana kuwa sayansi ama ustaarabu wa kiafrika ndio ustaarabu mkongwe kupita ustaarabu mwingine wowote ule katika sayari ya dunia.

Hata ustaarabu wa jamii mbalimbali duniani kama vile waajemi, wayunani (Ugiriki ya kale ), wamisri, wasumeri ( Mesopotamia/babiloni ) ya kale nakadhalika, unatokana na ustaarabu ambao msingi wake ni sayansi ya kiafrika.

• Sayansi ya kiafrika imethibitika kumsaidia mwanadamu katika kukabiliana na mazingira yake kwa zaidi ya asilimia tisini na tisa (99%).

• Kwa bahati mbaya sana, sayansi ya kiafrika imepewa jina baya kwa kuitwa uchawi na kupigwa vita mbaya tangu mamia ya miaka iliyopita, lengo kuu likiwa ni kumuondolea mwanadamu uwezo wa kiungu ulio wekwa ndani yake wa kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazo mkabili katika maisha yake ya kila siku.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Yaani nashindwa kuamini katika karne hii ya 20 kusikia mtu akiongea kama vile anaishi nyuma ya wakati. Kwenye maelezo yake ameshindwa kutueleza ni nini binaadamu atanufaika katika hizo faida za kujifunza UCHAWI ambazo amezielezea. Kwa mfano kuona viumbe visivyoonekana, kuzungumza na roho za watu walikufa au uwezo wa kupeleka heri na shari kwa binaadamu, je hivi vyote vina faida gani kwa binaadamu kama si kujirudisha nyuma. Kama angetueleza kwamba elimu yake ina uwezo wa kumfundisha mtu namna ya kuzidisha mazao shambani au kugeuza mchanga kuwa cement hapo tungeelewana. Acheni kuziba watu macho, huu sio mda wa kupotezeana wakati. Kupaa na ungo kutakusaidia nini?

    ReplyDelete
  2. huyu! anazungumza pumba hapa! ati sayansi ya kiafrika, hivi nayo hii unaita sayansi??? elimu ya kiza! hebu tumia hiyo sayansi ya kiafrika yenye historia ndefu kama unavyosema na kuweza kutatua matatizo ya mwanadam kwa asilimia 99% kututengezea angalau ka-boeing kaabiria tuweze kwenda arusha na kurudi, kweupe lakini maana unaweza kutuletea ungo halafu ati ndio uite Boeing!

    ReplyDelete
  3. Jana nilikuwa naangalia Documentary moja .. National Geaography channel , ilikuwa inahusu Aiport Dubai, sijui kama kuna mtu kashaoa hii Documentary, custom checking akatokea mwafrica kamatwa na vitu vya kichawi na michoro ya ajabu ambayo custom walisema michoro inatisha sana.. na mhusika, nilipata shock walipoosema kwamba anatokea mainland tanzania, the documentay was showing yeasterday and maybe will repeat thi weekend. wakasema hawaruhusi hivyo vitu kuingia na wataviaharibu na yeye atarudiswa Tanzania. i think was recorded 2012.

    ReplyDelete
  4. watanzania wachawi diamond ana pesa eti madawa ya kulevya yaani hatuamini kama mtu anaweza kufanikiwa bila uchawi au madawa. sad

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...