Malkia wa Zouk Hafsa Kazinja ameendelea kujizolea sifa toka kwa wadau wa muziki ndani na nje ya nchi baada ya kutoa wimbo wa NIMUOKOKE NANI Remix kama njia ya kumuenzi mkongwe Muhidin Maalim Gurumo aliyestaafu rasmi kazi ya muziki. 
Ngoma hiyo, iliyotengenezwa studio za OM Production chini ya wakali wa muziki wa dansi Omari Mkali na Abdul Salvador na ambayo imeanza kutamba katika vituo vya redion, inawakumbusha watu wazima miaka ya 70 wakati Gurumo alipotoa wimbo huo wenye kitenmdawili ambapo sasa vijana ambao ndio mwanzo wanausikia wameanza kukijadili kitendawili hicho huku wakiburudika na sauti nyororo ya Hafsa Kazinja, ambaye ametajwa kuwa ni jembe muhimu katika tasnia ya muziki kwa upande wa kinamama. Ngoma hiyo ya NUTA Jazz band ni kama kisafisha njia kwa nyimbo mpya za Hafsa ambaye anarejea uwanjani kwa kasi baada ya ukimya wa muda mrefu, akiendeleza pale alipoachia alipotoa ngoma ya PRESHA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...