Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na watumishi wa
Idara ya Uhamiaji Makao Makuu pamoja na wawakilishi wa idara hiyo Mkoa wa Dar
es Salaam (hawapo pichani) kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji kazi wa idara
hiyo. Kulia ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Kushoto ni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil pamoja na Kamishna
Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylvester Ambokile Mwakinyule. Dk
Nchimbi aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa uadilifu. Mkutano huo
ulifanyika katika ofisi za Uhamiaji Makao Makuu, jijini Dar es Salaam leo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na watumishi wa
Idara ya Uhamiaji Makao Makuu pamoja na wawakilishi wa idara hiyo Mkoa wa Dar
es Salaam. Dk Nchimbi alifanya ziara ya siku moja katika Ofisi
za Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam leo kwa lengo la kuzungumza
na watumishi hao masuala mbalimbali ya utendaji kazi..
- Kamishna wa Pasipoti na Uraia, wa Idara
ya Uhamiaji, Victoria Lembeli (kushoto) akimuuliza swali Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wa pili kutoka kulia) kuhusu
masuala mbalimbali ya maendeleo ya idara hiyo. Watumishi mbalimbali waliuliza
maswali pamoja na kutoa maoni yao katika mkutano huo uliofanyika katika
Ofisi za Makao Makuu ya idara hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam leo. Kulia
ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Kushoto (Meza Kuu) ni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil pamoja
na Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylvester Ambokile
Mwakinyule. (Picha na Felix Mwagara,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.).
Na vipi kuhusu KIMBUNGA? Mm binafsi sipo HAPPY na utekelezaji wa agizo la RAIS wetu,yani mm sielewi kabisa au hamkumuelewa nn alichokwambieni? Coz DAR ndio yenye wahamiaji wengi zaidi zile siku 14 alizotoa Muheshimiwa RAIS msichukulie kwenye hiyo MIKOA pekee bali ni NCHI NZIMA,kwa mtazamo wangu NYIE ndio mlio sababisha haya MATATIZO YOTE kwakua hamko MAKINI na KAZI ZENU,mpaka RAIS amekwambieni mko ZAIFU SN na hili halina kificho kwenu lipo wazi kabisa kwenu tena mshukulu Hajaivunja hii wizara,sasa bc tunataka kuona MSAKO NCHI NZIMA,na sehemu za kuanzia hizo hapo maana kila kitu nyinyi mnasubili mpaka muambiwe,MITAANI,MAHOTELINI,VIWANDANI,KWENYE MIGODI ya DHAHABU,KWENYE MASHULE,KWENYE MAMBUGA YA WANYAMA,na KWENYE WIZARA ZOTE,,ndugu zangu naomba nanyie mnisaidie sehemu ambayo labda mnaona sikuitaja,mm naitwa mdudu KAKAKUONA napatikana huku Uingereza,haya wadau kazi kwenu,na nawapendeni woote huko Nyumbani
ReplyDelete