Taasisi ya GS1 Tanzania kwa kushirikiana na Baraza la Uwezeshaji (NEEC) wamezindua mfumo wa ufatiliki wa asali ya Tanzania (Honey Traceability Project).
Sherehe za uzinduzi wa mfumo huo muhimu kwa bidhaa zinazozalishwa nchini umefanywa mjini Dodoma na Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyewakilishwa na Waziri wa Uwezeshaji Dr.Mary Nagu. Katika salamu zake kwa wadau Mheshimiwa Waziri Mkuu amewataka wasimamizi wa mfumo huo kuhakikisha unaanza mara moja ili kuiwezesha asali ya Tanzania iweze kuuzwa nje ya nchi na kuwanufaisha wakulima.
Kwa kuwa na mifumo hii, kutaziwezesha bidhaa za Tanzania zinaweza kuuzwa kama finished products nje ya nchi, kwani mifumo hii ua ufatiliki (Traceability System) inaweza kuonyesha historia ya bidhaa kuanzia ikiwa shambani, ilipopitia mpaka inamfikia mlaji, taarifa ambazo zikifuatiliwa zinapatikana kwa urahisi.
Awali Mkurugenzi mkuu wa GS1 Tanzania Bi. Fatma Kange alisema kuwa GS1 imejikita katika kutengeneza mifumo ya Ufatiliki (Traceability System) dunia nzima, tangu imeanzishwa miaka 40 iliyopita na kwa Tanzania mfumo huu ni wa kwanza wa kidigitali, kwani mpaka sasa ni mazao mawili tuu ya Tanzania ndio yamo kwenye mfumo wa ufatiliki ambayo ni Minofu ya Samaki na Mfumo wa Ufatiliki wa Kahawa.
Aidha akizungumza kwenye uzinduzi huo, mtaalamu wa mifumo ya Ufatiliki ya GS1 Tanzania Bw. Pius Mikongoti alisema kuwa Tanzania haina hiyari ya kuingia kwenye mifumo hii ya ufatiliki kwani kwa mujibu wa Sheria ya Chakula na MAdawa ya Jumuiya ua Ulaya, sheria no 78 ya mwaka 2002 inasema kuwa bidhaa zote zinazoliwa na binadamu ama mifuko katika jumuiya hiyo ni lazima ziwemo kwenye mifumo ya Ufatiliki ili ziweze kujulikana zilipotoka kuanzia mtengenezaji wa kwanza hadi zinapomfikia mlaji, hii ni katika kuzilinda haki za mlaji.
“Nia ni kuzalisha asali yenye viwango vya kimataifa hata kama ni ya kuliwa hapa hapa nchini lakini lazima iwe kwenye viwango ambavyo unaweza kuuza popote” alisema Bi. Kange
Naye Mheshimiwa Abdallah Kigoda, Waziri wa Viwanda na Biashara alisema kuwa kwa sasa sekta ya asali inakumbwa na changamoto nyingi ikiwamo ukosefu a vifungashio, masoko hafifu na vifaa vya urinaji na uchakataji wa kisasa, Kupitia wizara ya Viwanda na Bishara, serikali imefanikiwa kuongea na Kampuni kadhaa zikiwamo Kioo Limited na Omar Packaging ambazo zimekubali kuzalisha vifungashio maalumu kwa ajili ya zao hilo la asali.
Naye Mheshimiwa Nagu amesema kuwa Serikali kupitia baraza la Uwezeshaji na Wizara yake ya Uwezeshaji watahakikisha mifumo hii ya Ufatiliki inatengenezwa kwenye mazao yote ya Tanzania jambo ambalo litamaliza uuzwaji wa bidhaa ghafi sokoni.
Katika salamu zao kwa wadau kwenye uzinduzi huo Taasisi ya TPSF ambayo ni moja ya taasisi mama za GS1 imesema kuwa inajivunia kuona ndani ya miaka miwili tokea uanzishwaji wake Taasisi hii ya GS1 imeanza kuleta matunda stahiki kwa Watanzania, na hivyo kuahidi kuendelea kuisaidia taasisi hii na sekta binafsi kwa ujumla ili kuleta maendeleo ya TAifa kwa ujumla.
Nalo shirika la Viwango ambalo ni mmoja wa wadau na ndio waliofadhili uzinduzi hu mjini Dodoma wamesema kuwa kwa upande wao wameshatengeneza kiwango cha asali ambacho kinakubalika duniani kote na hivyo kuifanya kazi ya utengenezaji wa mfumo huo kuwa rahisi.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Wakuu wa Mikoa ya Katavi, Manyara, Dodoma, Singida na Tabora na Wakuu kadhaa wa Wilaya za mikoa husika, Wabunge, Wakurugenzi wa Maendeleo wa Mikoa na Wilaya, maafisa nyuki, na wadau mbali mbali wa nyuki hudu mashirika kadhaa yakiwakilishwa kama Word Vision, PASS, Shirika la Viwango la Taifa, Taasisi ya Sekta Binafsi, Benki ya Rasilimali, Taasisi ya NMB Foundations for Agriculture.
Mfumo huu kwa kuanzia umelenga mikoa Kumi ikiwamo Morogoro, Pwani, Tanga, Manyara, Dodoma, Singida, Katavi, Kigoma na Rukwa, na Tabora. Baada ya uzinduzi washiriki walipata nafasi ya kutembelea shamba la Mheshimiwa Waziri Mkuu lililoko endeo la Zuzu nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwezeshaji na Ukwekezaji, Dr. Mary Nagu akikata utepe kuzindua Mfumo wa Ufatiliki (Traceability System) wa Asali ya Tanzania, Wa kwanza kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Abdallah Kigoda, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anayeangalia kushoto kwa Waziri Nagu ni Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Elibariki Mmari na kushoto kwake ni Fatma Kange, Afisa Mtendaji Mkuu wa GS1 Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...