KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil amewataka wanamichezo wawakilishi wa wizara hiyo katika Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (Shimiwi) yanayofunguliwa rasmi Jumamosi mjini Dodoma wahakikishe wanaleta ushindi wa kishindo wizarani hapo.

Akizungumza na wanamichezo hao wapatao 140 kutoka Makao Makuu ya wizara hiyo pamoja na taasisi zake katika tafrija fupi ya kuwaaga wanamichezo hao iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Maafisa wa Polisi, Kurasini jijini Dar es Salaam jana, Abdulwakil alisema nidhamu, ushirikiano pamoja na ushirikiano utaleta ushindi wa kishindo katika mashindano hayo.

“Nawatakai ushindi katika michezo yenu yote mtakayoshiriki mjini Dodoma, ni matumaini yangu makubwa mtafanya vizuri kwani nimehakikishiwa hapa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kuwa tayari mmeshalipwa posho zenu za kujikimu hivyo tunahitaji ushindi tu,” alisema Abdulwakil.

Aidha, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa wizara hiyo, Nigel Msangi alilimuhakikishia Katibu Mkuu kuhusiana na posho za wanamichezo hao kuwa asilimia kubwa ya wanamichezo hao tayari wamelipwa na wachache watalipwa baada tafrija hiyo kumalizika.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Michezo wa Wizara hiyo, Florah Mwamadi alimuambia Katibu Mkuu kuwa mwaka huu timu zote za Wizara ya Mambo ya Ndani zimepewa maandalizi mazuri hivyo atarajie ushindi mkubwa pamoja na kupokea vikombe vyote vitakavyoshindaniwa katika mashindano hayo.

“Tunakuhakikishia tutapata ushindi na jiandae kupokea vikombe vyote, tumepjipanga vya kutosha na pia hatutarajii kupoteza mchezo hata mmoja katika mashindano yote tutakayoshiriki Shimiwi ya mwaka huu,” alisema Mwamadi.

Mashindano ya Shimiwi hufanyika kila mwaka ambapo inashirikisha watumishi wa serikali kutoka wizara zote pamoja na taasisi zake nchini ikiwa na dhumuni ya kujenga na kulinda afya za viongozi, watumishi, kuboresha mahusiano kazini, kujenga mshikamo kwa watumishi, kujenga utaifa na kuondoa utofauti baina ya watumishi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...