Juzi katika pita pita zangu nilisimama kidogo pale Quality Plaza ili nichukue pesa kidogo Bank kwa ajili ya sikukuu, cha kushangaza nilichokikuta baada ya kutoka tu Bank ndani ya dk 10 nikakutana na lundo la vijana wa NPS wakidai ushuru wa Parking!!! Nikajiuliza hivi hawa vijana wametokea wapi?? Mbona sijawahi kuwaona kipindi cha nyuma?? Na nikajiuliza tena hizi parking si za mwenye jengo?! Ila sikupata majibu ya maswali yangu wakati huo huo nilisikia watu wakisema mpaka wafanyakazi wa maeneo ya hilo jengo pia wanadaiwa ushuru wa parking ambao ni Tsh 300/= kila siku kwa saa.

Basi nikaondoka zangu nikiwa njiani nikakutana nao tena maeneo ya Jamana wametapakaa wengi saana ikionesha waziwazi ni ulaji wa mtu fulani na kawaweka pale kwa makusudi kabisa ya kutengeneza pesa!! Basi nikaelekea Uchumi Supermarket maana nilikuwa nimetoa pesa mwanzo ili niende kufanya shopping hapo...Kufika Uchumi Supermarket Quality Centre baada ya muda na kutoka nje wakati wa kuondoka tena nakutana nao wakidai tena pesa!! tena kwenye parking ambazo zimejengwa na mwenye jengo kwa mara nyingine tena!!!

Swali langu wadau hivi hawa watu wapo kwenye maeneo haya kisheria?? Je ni sahihi kutoza ushuru wa Parking kwenye maeneo ambayo yamejengwa na mwenye jengo?? Je haya maofisi na makampuni makubwa yaliyopo hapo kama CRDB Bank, DTB Bank, Stanbic Bank, Jamana Printers, Uchumi Supermarket, nk yanatueleza nini sisi wateja wao??? Je hizi ndio huduma bora wanazotupatia?? Maana tunawafuata wao kuwaletea business alafu tunachajiwa pesa kwa ajili ya parking ambazo wao wamepanga kwenye jengo hilo hilo!! Je sehemu kama Mlimani City Shopping Mall mbona wao hawacharge ushuru wa Parking??!!

Wahusika tunaomba mlifanyie kazi ili jambo na kutupatia majibu haraka iwezekanavyo maana huu ni wizi wa wazi wazi kwa wananchi fikiria ni Shilingi ngapi wanaingiza toka asubuhi mpaka jioni kila siku ya Mungu??!! na hatuoni faida ya hizo kodi!!! Yaani jengo ajenge mtu mwingine kodi wakusanye wao!!! Kweli haya ni majanga!!!!

WAHUSIKA TUNAOMBA MAJIBU.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. karibu bongo nchi ya wajanja wajanja

    ReplyDelete
  2. 16 October 2013 Last updated at 12:01 Share this pageEmail Print Share this page

    ShareFacebookTwitter.Hillary Clinton's Mercedes gets London parking fine

    Ndugu yangu pole huko Bongo, lakini soma hii kitu kwenye gazeti moja hapa Ukerewe jambo lililotokea jana.

    ReplyDelete
  3. no si haki yao hapo kunamendeo yaliyopo mjini ndio wanatakiwa kudai pesa za parking! wahusika tunaomba muiingile kati

    ReplyDelete
  4. Ya Quality siyajui lakini kulipia parking siyo jambo la ajabu siku hizi, ila nakubaliana na wewe malipo kama siyo ya halmashauri yawe yamehalalishwa na mwenye biashara. Jengo moja ambalo lilikuwa halilipii parking lilipoanza kulipia (mara moja tena wakitumia automatic machines kama za airport) niliuliza nikaambiwa waligundua parking zao zilikuwa zikitumiwa na watu wengine wasiohusika na biashara pale. Malipo ya masaa yalitumika kuwaondoa waliokuwa wanaacha magari yao pale kwa makusudi.

    ReplyDelete
  5. BONGO TAMBARALE NDIO!

    Mtoa Makala sasa wewe kama unavyoona hapo QUALITY PLAZA ni sehemu ya maisha ya juu hivyo usifikiri utaingia na Kupaki burebure kama upo Vichochoroni na kama unavyoona hapo juu Mdau wa UK amerusha Mama Hillary Clinton amelipishwa Gharama za Maegesho huko London!

    Unashangaa nini Kulipishwa Tsh.300/= kwa saa wakati Fedha unazo?, kwanza umetokea Bank na umevuta Mkwanja ATM sasa kwa nini usichangie Kidogo angalau wavuja jasho nao wakala?

    Kama ulifika Marekani maeneo ya Manhattan City centre ya New York City watu wanalipa hadi US$ 3,000 au zaidi kwa siku kwa maegesho leo unashangaa kulipa Tshs. 300/=kwa saa (SIO DOLLA ZA OBAMA) Fedha za Kikwete ?

    ReplyDelete
  6. Huyu mdau aliyeleta mada anaulizia uhalali wa malipo, vitajiri mbuzi vilipelekwa sijui ulaya/ marekani kwa kushikwa mkono kuhangaika na maisha vinaongelea thamani ya pesa, ndio maana maisha yenu ya kubahatisha kwa kutaka kuishi level ya juu msioiweza!

    ReplyDelete
  7. Sio sawa kulipishwa ktk maeneo ya Supamarket kama Q.Plaza,kwasababu wenye Maduka na Huduma zingine pale tayari wameshalipia kodi ya parkng kwa Manispaa husika. Na tukizidi kulifumbia macho hilo swala,hao hao watu wa NPS ndo wataanza kula sahani moja na vibaka ktk maeneo hayo.
    Uongozi wa Q.Plaza waliangalie hilo Swala kwa umakini zaidi.

    ReplyDelete
  8. Ni vizuri uchangie ajira ndugu yangu, hata parking attendant ni kazi, asipokula hapo ale wapi?

    ReplyDelete
  9. Ukiangalia moja ya mantiki husika na muhimu ya huu utaratibu wa kulipia maegesho ya magari, ni kuwashawishi wenye magari wasiongeze msongamano katikati mwa jiji/mji. Nyingine ni katika jitihada hizo hizo za kuwashawishi wenye magari na hii ni katika kuwabana wasihodhi maeneo ya maegesho kwa kuweka magari yao kwa muda mrefu na kuwanyima wengine fursa ya kutumia eneo hilo kuegesha magari yao pasipo kuwa na sababu maalum. Hii ya pili imelemea zaidi kwenye ubinafsi, ambao kwa kweli ni tatizo linaloongezeka huku kwetu Tanzania na Afrika kwa ujumla ambapo ukiangalia kiutamaduni, hatukuwa na tabia kama hiyo miaka ya nyuma.
    Tukiacha hayo, maeneo uliotaja yote ni kwa ajili ya huduma ambazo ni muhimu kwa raia na kwa kukuza uchumi wa nchi, halafu hayo ni majengo ambayo kwa ufahamu wangu, yamejengwa kwa huduma hizo maalumu kwa hiyo hao wenye majengo hawana budi kuweka maegesho ya magari bila tozo lolote kwa ajili ya wateja wao ambao wanawahitaji kibiashara.
    Tatizo sisi watanzania ni wapole na tumekuwa hatujui haki zetu za kimsingi halafu vilevile asilimia yetu kubwa tumekuwa tukiishi kiujanjajanja kwa hiyo mtu anaona 300 ndogo. Kutokana na hali hii tumekuwa tukichomekewa malipo kibao kutunyonya tu na yote ni mbinu za wachache ambao wanataka kuchota hata hicho kidogo cha wanyonge. Hawajui mtu umepigika vipi kulipata hilo gari la kukusaidia mizunguko yako ili uweze kupigana kupata riziki na kuchangia nchi katika kodi nyingine kibao. Hayo maeneo yote uliotaja hayatakiwi kulipiwa na mamlaka husika lazima wafuatilia hii kitu.

    ReplyDelete
  10. Hao jamaa ni wezi kabisa.

    ReplyDelete
  11. Kumiliki gari ni gharams,usingekuwa na gari nani angekuomba ushuru wa maegesho? Ulicho nacho gawana na wasiokuwa nacho,ndiyo uzalendo aliotuachia baba wa taifa

    ReplyDelete
  12. SHAURI ZENU NA HIYO MAREKANI YENU MAANA KILA KITU NAONA MNATAKA LINGANISHA NA MAREKANI. HAPA NI BONGO DAR ES SALAAM, FOR YOUR INFORMATION.SASA ULIFIKIRI UTAPAKI GAEI BURE? SWAIN WA BARAKA OBAMA.MSHAMBA NA MAREKANI YAKO!

    ReplyDelete
  13. Sasa unalalamika nini?unapesa za kununua gari lakini hutaki kulipa parking ya sh.300(Senti 20$)
    Cha kulalamika hapo ni kuwa kuwe na utaratibu wa kulipa na siyo watu 10 kuzunguka gari moja.

    ReplyDelete
  14. Nadhani hapa mwenye jengo itabidi atupe jibu.
    Tatizo nadhani linakuja kuwa hizo pesa zinazo kusanywa zinafanikisha lengo la kuboresha mji au jiji?
    Usilinganishe huko Marekani au Uingereza na bongo maana huko kila senti inahesabiwa na manufaa yake yanaonekana kwa wakazi wa mji au jiji husika, kwa mfano shule kuanzia primary mpaka high school ni bure na chai na chakula cha mchana kwa wanafunzi pia ni bure,na ipad au laptop ni bure.
    Hapa bongo tunalipa kodi lakini wajanja wengi, wanakabidhi 5% tu kwenye sirikali.
    Hii ni kero yetu na sio kuwa hatutaki kulipia kodi au parking,uwajibikaji hakuana,ni kuchakachua kwa kwenda juu

    ReplyDelete
  15. TATIZO TANZANIA WANAPENDA KUKUMBATIA WEZI NA HAWA JAMAA NI WEZI KAMA SIO MAJAMBAZI.WANASHERIA NA WAHUSIKA TETEA HAKI ZA RAIA!

    ZITO KABWE BABA INGILIA KATI ILI SWALA KAMA ULIVYOWAPIGA GAVANA VYAMA VYA SIASA.

    ReplyDelete
  16. dah hata mimi imenikuta na nilijiuliza sana hawa watu wanajua wanachofanya. sisi hatuoni shida kuwapa hiyo 300 ila tunataka maelezo mm nilijaribu kuwauliza tangazo hili limetoka wapi na limebandikwa wapi hawakuwa najibu sahihi. plz tunaomba wahusika walifanyie kazi kabla ayaaaaaaaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...