Rais Barack Obama amelihutubia taifa Jumatatu usiku akisiistiza kwamba jeshi la taifa litaendelea na kazi zake wakati sehemu za serikali kuu zinafungwa kuanzia leo Jumanne baada ya bunge kushindwa kukubaliana juu ya bajeti ya mwaka 2013 - 2014. Hatua hii inajulikana kama Government Shutdown.

Baada ya wabunge wa Baraza la Wawakilishi kushindwa kukubaliana ilipofika usiku wa manane Jumatau, juu ya bajeti ya matumizi, serikali kuu ililazimika kutangaza kwamba sehemu za idara kadhaa zitabidi kufungwa.
Mvutano wa kisiasa umekuwa ukiendelea bungeni kuhusiana na sheria ya kihistoria ya Rais Obama, ya kutoa huduma nafuu za afya ambayo imekuwa mashuhuri kwa jina la "Obamacare".
Baraza la wawakilishi linaoongozwa na chama cha Republican liliidhinisha mswada wa matumizi ya serikali lakini kwa kuambatanisha kufutwa kwa sheria ya Obamacare. Na mara tatu Baraza la Seneti linalodhibitiwa na chama cha Demokrat limepinga mswada huo.
Kutokanana Bunge kutokubaliana juu ya kupitisha mswada wa kuongeza muda wa matumizi ya serikali kuu sheria ya Marekani inahitaji idara zote ambazo hazina shughuli muhimu kusita kufanya kazi kuanzia Oktoba mosi, yaani leo Jumanne
Jumla ya wafanyakazi wa serikali wapatao 800,000 wanakwenda likizo bila malipo
ambapo inatarajiwa kutakuwa na hasara ya dola bilioni moja kwa wiki.
Chanzo:VOA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. This will give new life to DOOMSAYERS all over the world.There is this saying that all great nations eventually fall, and not in the hands of the enemy but from within.Its written in our history books. Nations fall, and sometimes those nations would have escaped but they did not, because they did not learn from history. One thing is, we never learn from history.Is this what is happening here? I hope not.

    ReplyDelete
  2. Sasa Kama America Itafanya "Government shut down" na Serikali ya Tanzania itafanya nini jamani na wao ndo watoa misaada wa kubwa duniani kooote? Sasa ndo dalili za mwisho wa Dunia kufika!!!!! Duu hili ni balaaa kubwa sana!!!!! America inayumba yumba sasa. God please save America and God please continue to save Africa.

    ReplyDelete
  3. Kumbe matatizo ni kila sehemu, hata marekani! mie nilidhani ni Tz tu!

    ReplyDelete
  4. Mzungu kama hujamfanya kuwa ndio mungu wako basi hupati mafanikio hapa dunia.

    ReplyDelete
  5. Bado kuna zile za kuwapa Syria ilikuondosha "silaha za sumu", operesheni za mashariki ya kati, vituo vya kijeshi kila pembe duniani, magereza ya Guantanamo na kengineyo, n.k. Hizi ndizo gharama za kuwa UNIPOLAR.

    Poleni sana.

    ReplyDelete
  6. Nafuu muandike kwa kiingereza msipoteze maana, bajeti ya mwaka 2013 - 2014 imetoka wapi? Hii siyo bajeti. Halafu congress siyo bunge.. Bunge ni parliament kuna tofauti ya utendaje.

    ReplyDelete
  7. Yote kwa Yote kiinglish ama si kiinglish inshu ni kwamba Amerika wanakwenda mrama. God Help Us All

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...