Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania -TRL  umetangaza kusitishwa kwa huduma ya treni ya jiji hapo kesho Jumatatu Oktoba 21, 2013 kufuatia ukarabati wa vichwa cha treni  vinavyotoa huduma hiyo kutokamilika kwa wakati.katika karakana ya Morogoro.
 
Taarifa za kufundi zimebainisha kuwa ukarabati wa vichwa hivyo utakamilika mapema kesho asubuhi na hivyo kuwasili  Dar jioni tayari kuanza huduma keshokutwa Jumanne, Oktoba 22, 2013 kwa mujibu wa ratiba yake ya kawaida..
 
Kuhusu kichwa cha treni kilichopata hitilafu ya kuungua moto jana jioni kikiwa safarini kutoka stesheni ya Kamata kuja kituo kikuu cha Dar ni miongoni  mwa ya vichwa vitatu vinavyofanyiwa ukarabati huko Morogoro.
 
Ukiwaomba radhi Wakazi wa jiji ambao ni watumiaji wakubwa wa huduma hiyo inayoanzia Stesheni ya Ubungo Maziwa hadi Stesheni ya Dar es salaam, Uongozi umewahakikishia kuwa mafundi wa TRL katika karakana za Morogoro na Dar es Salaam wanafanya kila jitihada kurejesha huduma hiyo kwa wakati ili kupunguza usumbufu kwa wateja.wake ambao wameizoeya sana huduma na kunufaika nayo.
 
Imetolewa kwa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu
 
Dar es Salaaam,
Oktoba 20, 2013

 
Midladjy Maez

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hii ni aibu kubwa katika huu ulimwengu wa leo...wezenu wako kwenye matreni ya mwendo kasi nyie ndio kwanza kila kukicha mnatuambia mambo ya ajabuajabu,,mnavizia MWAKYEMBE hayupo mnayumbisha mambo kimakusudi,,sisi wananchi hatutaki kusikia mambo ya kukarabati vichwa,,tunataka nyie mafundi muumize vichwa vyenu ili mtengeneze vichwa vipya vya matren na mabehewa mapya na ya kisasa zaidi,,nakama hamjui kutengeneza vitu vipya nini sasa maana ya kuitwa FUNDI? Haki ya mungu kwa mwendo huo hiyo TZ yetu maendeleo kamwe,,tutabaki kuitwa ni nchi ya DUNIA YA 3,,,na nyie mnaojiita mafundi kwenye hizo karakana za moro na dar mkija huku UINGEREZA mtaonekana ni vituko vya mwaka,,ndugu zangu msipende kujiita mafundi wakati hatakutengeneza au kubuni kitu kipya hujui so from today stop kujiita mafundi,,kwa jina naitwa mdudu kakakuona, nipo huku UINGEREZA,,na kama kuna mtu yeyote anataka kupewa ushauri wa aina yoyote ule nakuombeni ndugu zangu watanzania wenzangu msiogope kuulizia mawasiliano yangu kupitia hapa hapa kwa NDUGU MICHUZI,asanteni sn nakutakieni amani tele huko mliko nyumbani,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...