MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, jana imepiga kalenda kesi inayowakabili watu 11 akiwemo Diwani wa Kata ya Goba, Ibrahim Mohamed maarufu kama Kisoki, dhidi ya mashtaka 24 ya mauaji ya bila kukusudia yaliyotokana na gorofa 16 kuporomoka baada ya upande wa Jamhuri kudai kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Mbali na Kisoki washtakiwa wengine ni, Raza Ladha, Goodluck Mbanga, Willbroad Mugyabuso, Ibrahim Mohamed au maarufu kama Kisoki, Mohamed Abdulkarim, Charles Ogare, Zonazea Oushoudada, Vedasto Ruhale, Michael Hema, Albert Mnuo na Joseph Ringo.

Kesi hiyo iliahirishwa na Hakimu Mkazi Devota Kisoka baada ya upande wa Jamhuri kudai kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Wakili wa Serikali Petronila Kisaka alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kwamba jalada la kesi hiyo liko kwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi Ilala (RCO).

Hakimu Kisoka alisema kesi hiyo itatajwa tena Novemba 14, mwaka huu. Katika kesi hiyo, ilidaiwa kuwa Machi 29, mwaka huu mtaa wa Indrira Gandh, Wilaya ya Ilala washtakiwa kwa pamoja waliwaua watu 20 bila kukusudia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...