Kesi za unyanyasaji dhidi ya wanawake zinazidi kuwa nyingi. Wanawake wameendela kuumizwa na ubabe wa waume zao. Hivi karibuni, katika kijiji cha Kizanda wilayani Lushoto mkoa wa Tanga, mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Bi. Rahima alifariki dunia baada ya kupigwa na mumewe mateke ya tumboni angali mja mzito.

Taarifa za awali kutolewa zinasema kuwa mwanamke huyo alifariki kutokana na homa, lakini ndugu wa marehemu wamedai kuwa kifo cha ndugu yao kimetokana na kipigo. Bi Rahima ambaye alikuwa ni mja mzito, alifariki mwezi wa saba mwaka huu.

Taarifa za awali ambazo zilifikia Wanawake Live na Super Woman Joyce Kiria kufuatilia zilionekana kupita EATV usiku wa jana, na pia unaweza kufuatilia kwenye YouTube kupitia linki hii hapa chini ili ufahamu kile wanasheria wamekizungumza katika kutafuta haki kufuatia suala hili ambalo hata viongozi wa kijiji hicho wameshindwa kulitatua.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. vipindi kama hivi ni muhimu sana kuliko hata usanii wanaokalia wabunge kwani vinaendana na jamii halisi.You are super woman Big up Joyce.keep going tutafika

    ReplyDelete
  2. Tatizo la serkali Linachagua viongozi mrradi haizingatii, umuhimu wa jukumu analotakiwa kuwa nalo kiongozi hasa mashina kata kijiji mapaka ngazi za juu za uongozi. Mtu anachukuawa uongozi mradi kama pana masilahi apate mradi wake kwa kweli hatutafika kwa mpango kama huu serikali lazima iwe makini sana

    ReplyDelete
  3. Ivi huyu ni balozi anamuongoza nani huko Tanzania??????Mtu amekimbilia kwako baada ya kupigwa na mumewe,wewe kama kiongozi hatua uliyochukua ni kumwambia lala hapa!Ama kweli tuna safari ndefu sana.Amenikera huyu mwanamke,Napata picha ya hiyo jamii anayoiongoza hapa kijijini kwake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...