Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amezipongeza kampuni za usafirishaji ambazo zina rekodi ya kutozidisha uzito katika magari yao zadi ya viwango vilivyowekwa kisheria. Waziri Magufuli alielezea hayo wakati alipokutana na Waandishi wa Habari mapema wiki hii.
“Kumbukumbu zilizofanyiwa uchambuzi kwa kipindi cha miaka kumi zimebainisha kuwa yapo makampuni ambayo hayana rekodi ya kuzidisha mizigo wakati wote yanapopimwa katika vituo vya mizani ya barabarani” alibainisha Waziri Magufuli huku akisistiza kuwa kampuni za aina hii hazina budi kupongezwa kwa uzalendo na kwa kuzingatia weledi katika uendeshaji wa shughuli zao.
Kampuni za usafirishaji alizozitaja kuwa mfano wa kuigwa ni pamoja na; Dar Express, Cargo Star, Hood bus, Coca Cola, BM Coach, Bakhresa (AZAM Transport), TBL, Golden Coach, Kanji Lanji Co. Ltd, Taqwa, Consolidated Logistic, Lamada, na BP ambayo kwa sasa inaendeshwa na Puma.
Aidha katika hatua nyingine, Waziri wa Ujenzi amebainisha kuwa katika kipindi cha hivi karibuni Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) ulifanya zoezi maalum la kutangaza upya ajira za watendaji katika vituo vyote vya mizani ya barabarani hapa nchini. Katika zoezi hilo wafanyakazi takriban 400 ambao ni sawa na asiliamia 85 ya watumishi wote katika vituo hivyo walibadilishwa.
Hatua ya kubadilishwa kwa watendaji hao inaelezwa kuwa ni chanzo kingine cha malalamiko kutoka kwa baadhi ya wasafirishaji wasio waaminifu waliokuwa na mawasiliano ya karibu na watendaji wa zamani waliokuwa wakishirikiana nao kupitisha mizigo  kinyume na taratibu. Mianya hiyo kwa sasa imezidi kudhibitiwa.
Mheshimiwa Magufuli ameendelea kuuhakikishia umma kuwa wizara yake itaendelea kusimamia sheria ili kuhakikisha kwamba jitihada zinazofanywa na Serikali hazidhoofishwi na watu wachache wenye nia ya kujinufaisha binafsi bila ya kujali maslahi ya Taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Wengi wetu tunapenda sana kuhusisha sheria na siasa.
    Asiyefuata sheria aache hiyo biashara.Kwanza serikali ianze kasi ya kuimarisha reli,hata bidhaa zitashuka bei.
    Reli ikifanya kazi viburi vya wenye malori zitaisha.

    ReplyDelete
  2. kama tungekuwa na kiburi ungekula nini reli tumepewa bure na mkoloni na tumeshindwa kuiendesha ,tunashidnwa ku endesha tazara, wacheni ushabiki ,waziri huyo huyo amevunja manyumba za watu na kunyanyasa watu na ni nani mtanzania yuko juu ya sheria. ushabiki acheni

    ReplyDelete
  3. wenye lori hatuna viburi
    reli tulipewa bure na mkoloni tumeshidwa kuiendeleza,tazara nae hivyo hivyo, tu ache ushabiki elewa nini kina zungumzwa halafu ndio uchangie hoja

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...