Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika kitabu cha maombolezo ya Askofu Mstaafu, Mhasham Raymond Mwanyika, wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika leo katika Kanisa Katoliki Njombe.
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Spika Anne Makinda na viongozi wengine wakielekea kanisani kuaga mwili wa marehemu
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Spika Anne Makinda na viongozi wengine wakitoa heshima za mwisho na kuaga  mwili wa marehemu
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka mchanga kaburini
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Katibu Kiongozi Mstaafu Mhe Philemon Luhanjo baada ya mazishi hayo. Picha na OMR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. 2015: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.

    ReplyDelete
  2. R.I.P. Askofu Mstaafu, Mhasham Raymond Mwanyika.

    Wahusika tafadhali, haya matukio katika picha, nadhani ni vizuri zaidi mkawa mnayaweka kimpangililio kwa kuzingatia ni tukio lipi la mwanzo, lipi linafuata na lipi linamalizikia. Hapa katika picha ya pili, tunamuona Mh. Makamu Wa Rais Dkt. Bilal akiweka shada la maua juu ya Kaburi, kisha picha ya tano hapo chini akiweka mchanga kaburini, Ni vizuri picha za matukio mbali mbali mnapozitoa, zingatieni kimeanza kipi, kikafuatia nini na kuishia na kipi,

    Mfano hapo ingeanza ya Kwenda kanisani, kusaini Kitabu, kuaga mwili, kuweka mchanga na hiyo ya kusalimiana kama ilivyo ya mwisho. ( Ni mawazo na ushauri tu).

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...