Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza katika harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa kanisa la Moravian Tanzania mjini Sumbawanga akimuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda aliyemteua kufanya hivyo baada ya yeye kukabiliwa na majumu mengine ya kitaifa. Awali Waziri Mkuu aliafiki mualiko wa Kanisa hilo katika kuongoza harambee hiyo ambayo imefanikiwa kupata zaidi ya Tsh. Milioni 58 zikiwepo fedha taslim zaidi ya shilingi Milioni 47 na nyingine zikiwa ni ahadi. Zimekuwepo pia ahadi za mifuko 30 ya Cement na mlango mmoja mkubwa wa kuingilia kanisani hapo.
Askofu Mkuu Conerad Nguvumali wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Rukwa akitoa neno katika hafla hiyo ambayo aliwataka waumini wa kanisa hilo kuchapa kazi kwa nguvu na kuepukana na uvivu ambao alisema ni ugonjwa mkubwa kuliko hata gonjwa la ukimwi. Alikemea pia tabia ya watu wengi kuwahusisha watu waliofanikiwa kwa jitihada zao wenyewe na imani za "Freemason" au "Ufisadi".
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka akizungumza katika harambee hiyo baada ya kupewa fursa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kutoa mchango wake, aliahidi mchango wa laki tano na mlango mmoja mkubwa wa kuingilia kanisani hapo.
Baadhi ya viongozi wa Serikali waliohudhuria katika hafla hiyo, kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga William Shimwela ambaye pia ni mwanakamati wa ujenzi katika kanisa hilo, Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hillal na nyuma yake ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa Mwaruanda.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiendelea na zoezi la uchangishaji.
Baadhi ya waumini wa kanisa la Moravian Sumbawanga wakimfagilia kwa shangwe Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hillal aliyachangia Tsh. Milioni kumi zikiwepo za kwake binafsi Mil. 7 na nyingine Mil. 3 kuchangiwa na wabunge wenzake.(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)








Hongera mama Stella nakusifia sana kwani unapokwenda kwenye shughuli za dini basi unavaa ipasavyo.
ReplyDeletePlease keep it up