Mpambano huo utakaopigwa nchini China   November 30, 2013   Mchina Xiong Zhao Zhong ambaye ni bingwa wa dunia wa WBC ambaye anashikilia taji hilo kwa sasa katika uzito huo
Kimweri anakuwa mtanzania wa kwanza kuwania taji kubwa kabisa Duniani akitokea nchini Austalia. 
Omari Kimweri
na Randy petalcoria
Kigezo cha kufanya apate pambano hilo kubwa ni kutokana na rekodi yake pamoja na kutakiwa mtu ambaye anatokea bara la Afrika ambapo kura imemdondokea bondia Omari Kimweri, ambapo ni kiu ya mabondia wengi duniani kumiliki mikanda mikubwa ya kimataifa. Kimweri mwenye rekodi  ya kucheza michezo 16 ambapo ameshinda michezo 13 na kuchezea kichapo michezo 3  wakati mpinzani wake   Xiong Zhao Zhong amecheza michezo 26 akishinda 21 kupigwa 4 na kutoka droo moja.

Mabondia hao wote wana umri wa  miaka 31, wakitofautiana kwa mwezi mmoja tu katika kuzaliwa. Mpambano wao umekuwa gumzo katika dunia ambapo kila mmoja anajiandaa kwa nguvu 

Kimweri kwa sasa anaefanya mazoezi makali, akipewa sparring na bondia  Randy Petalcoria  wa Philippines ambaye ni bingwa wa  light fly weight.
Omari Kimweri kwa sasa yupo katika mazoezi mazito ya kujiandaa na mpambano huo, akitegemea zaidi dua za Watanzania kwa kuwa ushindi wake ni ushindi wa watanzania wote.
 Mungu Ibariki Tanzania 
Mungu Mbariki Bondia Omari Kimweri

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ndio yale yale yaliosemwa juzi juzi hapa, watu mnamdandia na kumuita mtanzania, ilhali amechukua uraia wa nchi nyengine. Kwa kuwa tu anafanya jambo la kijivunia kila mmoja anamwita mtanzania, lakini wakati huo huo hamtaki kuwapa uraia wa nchi mbili ha ha ha!!!!!

    Ngojeeni wakati akipanda ulingoni ni muziki wa taifa gani utapigiwa :)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...