UONGOZI wa Mkoa wa Mwanza umeupongeza Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa uamuzi wake wa busara wa kujenga Kituo cha Polisi eneo la PPF Kiseke, ambapo Mfuko huo ulijenga  jumla ya nyumba 580 na kuuzia wananchi kwa sh. Milioni 22 hadi 36 kwa kutegemeana na ukubwa.

Pongezi kwa Mfuko huo zilitolewa mjini hapa jana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Ndaro Kulwinjira, katika hafla ya kukabidhi kituo hicho cha polisi kwa uongozi wa mkoa wa Mwanza. “Kitendo hiki kinaunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na uhalifu, ili uweze kupambana na uhalifu lazima uwe na askari, vitendea kazi na sehemu ya kufanyia kazi ambayo leo hii PPF mmetupatia,” alisema na kuongeza kuwa;

“PPF imekuwa karibu sana na sisi, PPF Mwanza mnatusaidia sana katika juhudi za kupambana na uhalifu, kwa sasa mkoani hapa hali ni nzuri tofauti na zamani na tunsingefika hapa bila kushirikiana na wadau.”
Alisema PPF imekuwa na mchango mkubwa  wa maendeleo ya mkoa wa Mwanza. “Hapa wamejenga nyumba 580 na bado wanataka kujenga zingine, wameona hiyo haitoshi wamejenga kituo cha polisi kwa sh. Milioni 49.5, hizi ni fedha nyingi wangeweza kuwekeza sehemu nyingine,” alisema Kulwinjira.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio (Kushoto) akishirikiana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Ndaro Kurwijila (Wapili kulia) kufunua kitambaa ikiwa ni ishara ya Uzinduzi wa jengo la kituo cha polisi kijiji cha PPF Kiseke, wilayani Ilemela mkoa wa Mwanza jana.Wanaoshuhudia ni Kamanda wa Polisi wa wilaya hiyo (OCD), Deborah Magiliginda (Kushoto) na Kulia ni Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Joseph Konyo. Ujenzi wa kituo hicho uliogharimu shilingi milioni 49.5, ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya PPF, kujenga kituo cha polisi kwenye kijiji hicho ambako Mfuko huo ulijenga nyumba 580 na kuziuza kwa wananchi.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Ndaro Kurwijila (Wapili kulia), kwa niaba ya Mfuko wa Pensheni wa PPF akipena mikono na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Joseph Konyo, ikiwa ni ishara ya kumkabidhi jengo la kituo cha polisi kijiji cha PPF Kiseke, wilayani Ilemela mkoa wa Mwanza jana na kushuhudiwa na Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio (Kushoto) na Kamanda wa Polisi wa wilaya hiyo (OCD), Deborah Magiliginda (Kulia). Ujenzi wa kituo hicho uliogharimu shilingi milioni 49.5, ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya PPF, kujenga kituo cha polisi kwenye kijiji hicho ambako Mfuko huo ulijenga nyumba 580 na kuziuza kwa wananchi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (Aliyesimama), akitoa hotuba wakati akikabidhi jingo la kituo cha polisi kijiji cha PPF Kiseke wilayani Ilemela mkoa wa Mwanza jana. Ujenzi wa kituo hicho uliogharimu shilingi milioni 49.5, ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya PPF, kujenga kituo cha polisi kwenye kijiji hicho ambako Mfuko huo ulijenga nyumba 580 na kuziuza kwa wananchi. Wengine pichani kutoka kushoto, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko huo, Steven Alfred, Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Jeseph Konyo, Kaimu mkuu wa mkoa wa Mwanza, Ndaro Kurwijila na kamanda wa polisi wilaya ya Ilemela (OCD), Deborah Magiliginda.
Kamanda wa polisi wilaya ya Ilemela (OCD),Mkoani Mwanza, Deborah Magiliginda, (Aliyesiamama), akitoa hotuba yake kwenye hafla ya kupokea jengo la kituo cha polisi kijiji cha PPF Kiseke mkoani humo jana.Ujenzi wa kituo hicho uliogharimu shilingi milioni 49.5, ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya PPF, kujenga kituo cha polisi kwenye kijiji hicho ambako Mfuko huo ulijenga nyumba 580 na kuziuza kwa wananchi.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...