Mmoja wa watalii akijikuta akiingia katikati ya ngoma za utamaduni baada ya kunogewa na ngoma ya Msewe maarufu kama 'Kibati' siku ya Utalii Duniani iliyoadhimishwa Zanzibar.
Ngongoti huyu akiwa mmoja wa kiburudisho katika sherehe hizo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh. Ali Juma Shamuhuna akifunguwa resi za ngalawa Foroza Mchangani mjini Zanzibar.
Ngalawa zikionekana kuanza resi hizo siku ya Utalii Duniani .
Mshindi wa mwanzo wa ngalawa ya Lailati Bw Khalidi Khamis akipokea zawadi kwa mgeni rasimi Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh Ali Juma Shamuhuna.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...